Å·±¦ÓéÀÖ

Eliya Quotes

Quotes tagged as "eliya" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Wafuasi wa Yesu Kristo watapata taabu kubwa ambayo haijawahi kutokea. Yeyote atakayempinga Mpinga Kristo, yeyote atakayepinga utawala wa Mpinga Kristo, atakiona cha mtema kuni. Watu wengi watauwawa kwa sababu ya ufuasi wao kwa Masihi. Wale watakaokuwa na talanta ya kuhubiri watauwawa kinyama, hadharani, ili liwe fundisho kwa wafuasi wengine wa Yesu Kristo.

Miongoni mwa wale watakaokuwa wanahubiri injili ya kweli ya ufalme wa Mungu bila woga wa aina yoyote ile, atakuwemo Eliya na Enock. Eliya na Enock Mungu aliwachukua bila kuonja mauti, kama akiba, kwa sababu ya kipindi hicho cha Taabu ya Yakobo.

Eliya na Enock wataibuka ghafla jijini Yerusalemu na kuanza kuhubiri injili ya kumpinga Mpinga Kristo. Kwa vile hawataogopa chochote, wala hawatamwogopa yeyote, serikali ya Israeli itawakamata na kuwatesa lakini hawatanyamaza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mpinga Kristo atakapoona imeshindikana kuwanyamazisha, Eliya na Enock, huku akitamba kwamba yeye ndiye Yesu Kristo ambaye kila mtu ndiye aliyekuwa akimsubiri arudi kwa mara ya pili; na kwamba yeye anatoka katika ukoo wa mfalme Daudi, ili watu waamini kama kweli yeye ndiye Yesu Kristo, ataamuru Eliya na Enock wauwawe hadharani kama wahubiri wengine.

Eliya na Enock watakapouwawa, Mungu atawafufua na watarudi mbinguni wakiwa wameonja mauti kama binadamu mwingine yeyote yule. Hapo mlango wa rehema utakuwa umefungwa. Muda wowote kuanzia hapo Yesu atarudi, kwa mara ya pili, na kwa ajili ya ufufuo wa kwanza.”
Enock Maregesi