欧宝娱乐

Mzazi Quotes

Quotes tagged as "mzazi" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Watoto hupenda vitu vinavyong鈥檃a ambavyo havijatulia na vilivyopangiliwa vizuri. Hivyo ndivyo macho ya binadamu yalivyo: yana unyevu na yanaakisi mwanga, hayajatulia, na yana rangi kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kope na vigubiko vya macho ambavyo pia hazijatulia. Mtoto mchanga hasa yule anayeona vizuri huangalia macho pale anapopata nafasi, kwa maana ya kuyashangaa. Vilevile, huangalia macho kwa maana ya kupokea molekuli ya maadili au homoni inayorahisisha maisha kutoka kwa mama yake iitwayo 鈥榦xytocin鈥�. 鈥極xytocin鈥� husisimua ubongo wake na kuutayarisha kupokea neno lolote litakalosemwa na mama yake mzazi au mama yake mlezi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mzazi hamjui mtoto wake na mtoto hamjui mzazi wake. Kila mtu hapa duniani ni wa kipekee na wanasayansi wanatuambia kuwa tuko peke yetu hapa ulimwenguni. Lazima tujifunze kupendana na kuheshimiana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiitwa mtoto kidini ina maana una imani na unyenyekevu mbele ya Mungu, kama ambavyo mtoto ana imani na unyenyekevu mbele ya mzazi wake. Lakini ukiitwa mtoto kidunia watu watakudharau.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mzazi wako akikwambia kuwa usiwe mkorofi, usivunje sheria za nchi, usiwe na marafiki wabaya, na usiasi dhidi ya serikali, mheshimu kwa kukubali. Akikwambia kuwa uwe mkorofi, uvunje sheria za nchi, uwe na marafiki wabaya, na uasi dhidi ya serikali, mheshimu kwa kukataa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mzazi wako akikutuma kufanya jambo jema ukakubali umemheshimu. Akikutuma kufanya jambo jema ukakataa umemdharau. Lakini, mzazi wako akikutuma kufanya jambo baya ukakubali umemdharau. Akikutuma kufanya jambo baya ukakataa umemheshimu. Hivyo, mheshimu mzazi wako katika mambo mema na katika mambo mabaya.”
Enock Maregesi