Å·±¦ÓéÀÖ

Msaada Quotes

Quotes tagged as "msaada" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Wewe kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, ‘Mungu umeshindwa hebu ngoja na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John Doe.â€� Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye utakayemtatulia matatizo yake. Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, ‘Usiwe na miungu mingine ila mimi.â€� Kuingilia mambo ya John tayari umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake. Mungu akikuruhusu kuingilia kati, yaani John akiamua kwa hiari yake mwenyewe kukuomba msaada wa mawazo au ushauri, maana yake ni kwamba Mungu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya mafanikio ya John Doe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hutaweza kufikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu â€� Hata kama una kipaji au ujuzi kiasi gani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Vitibegi vya makomandoo wa Tume ya Dunia (vitibegi vya msalaba mwekundu na vitibegi vya kujiokolea) vilikuwa na vifaa maridadi vya kisasa kama vile pisto, visu, madawa ya huduma ya kwanza, kalamu za Inka, ramani za Meksiko, tochi ndogo zenye mwanga mkali za Cyba-Lite, Vioo vya TOPS, vibiriti vya Firesteel, pasi za kusafiria, pesa na vipenga vyenye viwango vya sauti vya desabo 126. Kipenga chenye kiwango cha sauti cha desabo 126 kinaweza kupasua ngoma za masikio ya adui, na kuwajulisha Vijana wa Tume mwenzao alipo hivyo kwenda haraka na kumpa msaada.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maana halisi ya ukarimu si kutoa vitu au mali nyingi kwa watu wanaohitaji msaada, bali ni kutoa vitu au mali hizo bila kinyongo au unafiki wowote. Ukarimu unapaswa kutolewa kwa watu sahihi, wakati sahihi, kiasi sahihi na kwa moyo mmoja bila kinyongo chochote. Ukitoa kwa lengo la kupata faida, huo ni ubinafsi na unafiki mkubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukimpa msaada uliyemkosea unammaliza.”
Enock Maregesi