Å·±¦ÓéÀÖ

Maisha Quotes

Quotes tagged as "maisha" Showing 1-30 of 94
Enock Maregesi
“Mungu akikubariki kipaji chako watu watasema ni laana. Maisha yako ni sawa na mto. Unakoelekea ni baharini. Lakini sasa umefika kwenye mlango wa bahari. Unahangaika upite wapi kufika baharini, ambapo utaogelea kwa kadiri utakavyoweza. Utakapofika baharini, watu, badala ya kusema umebarikiwa, watasema umelaaniwa, badala ya kukuita malaika, watakuita shetani. Mafanikio hayapimwi kwa pesa au mali kiasi gani unayo, mafanikio yanapimwa kwa amani ya moyo au maisha ya watu kiasi gani umeboresha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usiingilie mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako â€� ya mwingine Mungu anayafanyia kazi â€� hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, acha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama John Doe ana matatizo katika maisha yake acha ayatatue mwenyewe. Akishindwa atakuomba ushauri au ataomba ushauri kutoka kanisani kama ni Mkristo, au msikitini kama Mwislamu, au kutoka katika nyumba yoyote ya ibada kulingana na imani yake. Mtu akikuomba ushauri mshauri kwa moyo wako wote, wala usimshauri kwa unafiki au kinyongo cha aina yoyote ile.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wewe kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, ‘Mungu umeshindwa hebu ngoja na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John Doe.â€� Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye utakayemtatulia matatizo yake. Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, ‘Usiwe na miungu mingine ila mimi.â€� Kuingilia mambo ya John tayari umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake. Mungu akikuruhusu kuingilia kati, yaani John akiamua kwa hiari yake mwenyewe kukuomba msaada wa mawazo au ushauri, maana yake ni kwamba Mungu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya mafanikio ya John Doe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usipokula maisha maisha yatakufanya chakula.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mahatma Gandhi alipigwa risasi na kufariki dunia baada ya maisha yake kumfelisha. Lakini kifo chake kiliipatia India uhuru kutoka Uingereza. Hivyo, akafanikiwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu wakati anakufa msalabani hakufikiria kifo. Alifikiria maisha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna maisha baada ya saa tisa na nusu. Kuwa makini na raia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Katika maisha ni vigumu kupata jibu sahihi kwa akili yako mwenyewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Katika Biblia kuna tabiri 333 kuhusu maisha ya Yesu Kristo, na kuhusu kurudi kwake kwa mara ya pili. Kati ya hizo, 332 zilitimia! Bado mmoja tu: Kurudi kwa Yesu Kristo kwa mara ya pili.

Unadhani huo wa kurudi kwa Yesu Kristo kwa mara ya pili hautatimia? Muda umefika. Jitathmini katika maisha yako na uchague lililo jema.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu anatupenda sana, ndiyo maana akamleta Mwanawe wa pekee ili afe kwa ajili yetu, lakini haupendi mfumo wa maisha wa dunia hii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“ATP hutumika katika kipindi ambapo mtu anakuwa amekata tamaa kabisa katika jambo lolote analolifanya, na yeyote anayetumia ATP ana uwezo mkubwa wa kufanikiwa katika maisha yake. Hivyo, usikate tamaa, jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiua mtu damu yake itakusuta maisha yako yote! Itaongea na wewe ikikulaumu milele!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu alikupa maisha akakupa akili ili utambue jema na baya na akakupa amri zake ili uishi kwa amani na upendo. Kama Mungu hayupo mwanamume na mwanamke walitoka wapi? Wazazi wako walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi?”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kinachotokea katika dunia hii si kitu kizuri cha kuzoea au hata kufikiria. Hivyo tuna haki ya kuwa na mawazo, hasira na wanyonge kuhusiana na suala zima la maisha yetu hapa duniani. Hata hivyo hali hii itabaki kuwa hivyo kwa sababu Mungu ametaka iwe hivyo kwa sasa. Kwa maana hiyo, hekima ni kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Lazima tukubaliane na kisichoweza kufikirika kuweza kubadilika.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ubatizo ni toba iletayo ondoleo la dhambi. Mwangushe Goliati wa uzinzi katika maisha yako kwa kumtumia Yesu Kristo, ambaye ni Daudi wa mapandikizi yote ya dhambi katika maisha yetu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuishi na watu vizuri ni ufundi mkubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nuhu anasemekana kuwa mtu aliyedharaulika sana huko Babeli. Maisha yake yalijaa utata. Lakini ukweli ni kwamba, bila Nuhu mimi na wewe tusingekuwapo. Unayemdharau sana mwogope sana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kabla hujapona matatizo yanayokusumbua ponya roho yako kwanza, kabla hujakwenda kwa mchungaji, roho yako inajua kila kitu katika maisha yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hakuna uponyaji pasipo imani ya kweli. Giza linapoingia katika maisha yako ongea na Mungu. Halafu ongea na tatizo linalokusumbua. Kama tatizo linalokusumbua ni saratani, iambie saratani iondoke na kamwe isirudi katika mwili wako tena. Baada ya hapo, nenda kwa mchungaji. Jiweke wakfu, kwanza, kabla ya kuombewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maisha yangu ni kafara ya mafanikio yangu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitaka kuishi usiogope kufa. Kwa maneno mengine, ukitaka kufanikiwa katika maisha yako, usiogope kufa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna watu hawaamini kama Mungu yupo, lakini maisha yao yanaamini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni kilichowashangaza hata wanasayansi wa dunia hii. Amka na uujue ukweli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kujiponya kisaikolojia lazima unyanyuke kiroho hadi katika ulimwengu wa roho, na uyatazame maisha yako kutokea juu kuja chini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu aliishi maisha yake yote chini ya utawala wa kidikteta lakini hakuandamana. Kwa nini sisi leo?”
Enock Maregesi

“Kila mtu anajaribu kuwa mwema lakini maisha tunayoishi yanatufanya kuwa sisi. ”
Chrisper Malamsha

Enock Maregesi
“Maisha ni Dunia. Lakini Dunia ni basi. Sisi ni wasafiri. Mtu anapokufa amefika mwisho wa safari yake, huku Dunia ikiendelea.”
Enock Maregesi

“Mtu hujichorea ramani yake ya maisha mwenyewe.”
Pauline Kea, Kigogo
tags: maisha

« previous 1 3 4