Å·±¦ÓéÀÖ

Nyuma Quotes

Quotes tagged as "nyuma" Showing 1-6 of 6
Enock Maregesi
“Katika nyuma geuka ya gwaride, wa kwanza anakuwa wa mwisho, wa mwisho anakuwa wa kwanza. Geuka, ukifika mwisho wa njia. Huo ndiyo mwanzo wa njia nyingine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Murphy alichanganyikiwa. Hakujua nini kilitokea na kwa nini. Ila, ghafla, alipotupa macho kushoto aliona kitu. Joka kubwa lilitambaa, ingawa kwa shida, kwa sababu ya sakafu, na kumfuata kummaliza. Murphy alijua joka hata angefanya vipi, hakuwa na uwezo wa kujikinga. Alipotaka kupiga kelele ili walinzi wa nje waje, Murphy alishindwa. Nyuma ya joka â€� katika mkia â€� kuna kitu kiling’aa, kikamshangaza! Muujiza ulimtokea Murphy lakini kitu kikamwambia aite walinzi wa nje ili waje wamuue yule nyoka. Lakini kabla hajapiga kelele, alisikia sauti; si ya mwanamume. Ya mwanamke!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Murphy hakupenda kupoteza muda. Alinyanyuka na kumimina risasi, Mungu akamsaidia akadondosha wawili huku wengine wakipotea kwa kuruka vibaya na kukwepa. Kwa kasi Murphy alikimbia huku ameinama mpaka katika milango mikubwa ya nje, ambayo sasa ilikuwa wazi. Hapo akasita. Chochote kingeweza kumpata kwa nje kama hangekuwa mwangalifu. Bunduki yake ilishakwisha risasi. Aliitupa na kuchungulia nje akaona adui mmoja akikatisha kwenda nyuma ambako ndiko mashambulizi yalikokuwa yakisikika sasa. Murphy hakumtaka huyo. Aligeukia ndani kuona kama kulikuwa na bunduki aichukue lakini hata kisu hakikuwepo. Akiwa bado anashangaa, ghafla alitokea adui â€� kwa ndani â€� na kurusha risasi, bahati nzuri akamkosa Murphy. Murphy, kama mbayuwayu, aliruka na kusafiri hewani hapohapo akadondoka nyuma ya tangi la gesi karibu na milango ya nje. Alipoona vile, adui alidhani Murphy alidondoka mbali. Alibung’aa asijue la kufanya. Wasiwasi ulipomzidi alishindwa kuvumilia. Alishika bunduki kwa nguvu na kupiga kelele, "Yuko hukuuu!" Halafu akajificha ili Murphy asimwone. Lakini Murphy alikuwa akimwona.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Simama nyuma ya maneno yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukikaa nyuma yangu utafanikiwa, ukikaa mbele utaanguka.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unapokwenda mbali na Mungu, ili umrudie lazima urudi nyuma.”
Enock Maregesi