Å·±¦ÓéÀÖ

Rais Wa Meksiko Quotes

Quotes tagged as "rais-wa-meksiko" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Peter, naomba nitubu kosa. Mimi si mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ni mtoto wa Rais wa Meksiko. Lisa ni mtoto wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,â€� Debbie alisema akitabasamu.
“Hata mimi nilijua ulikuwa ukinidanganya. Lakini mbona Rais wa Meksiko haitwi Patrocinio Abrego?� Murphy aliuliza.
“Utamaduni wa Meksiko ni tofauti kidogo na tamaduni zingine,â€� Debbie alijibu baada ya kurusha nywele nyuma kuona vizuri. “Hapa, watu wengi hawatumii majina ya pili ya baba zao. Hutumia jina la kwanza la mama la pili la baba; ndiyo maana Wameksiko wengi wana majina matatu. Kwa upande wangu, Patrocinio ni jina la baba yake mama yangu na Abrego ni jina la babu yake mama yangu â€� kwa sababu za kiusalama.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kesho yake Ijumaa Rais wa Meksiko alirudi kutoka Panama na aliomba kuonana na Vijana wa Tume; alitaka kuwapongeza binafsi, na kuwapa nishani za heshima kwa mchango wao mkubwa kwa Jamii ya Meksiko. Randall Ortega alilipeleka ombi hilo kwa Rais wa Tume ya Dunia; Rais wa Tume ya Dunia akakaa na Kamati ya Usalama ya Tume ya Dunia na kumrudishia Randall Ortega jawabu, kwamba Vijana wa Tume waliruhusiwa kuonana na Rais wa Meksiko na baadhi ya maafisa wa juu wa serikali ya shirikisho. Saa mbili usiku wa siku hiyo, Ijumaa, kulifanyika sherehe ndogo ya siri nyumbani kwao Debbie; sherehe iliyohudhuriwa na Rais wa Meksiko na mke wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Meksiko, Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya Nchini Marekani, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu Nchini Meksiko, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, maafisa wa tume na watu wengine wa muhimu katika kazi ya Vijana wa Tume.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kilometa mbili na ushei kidogo kutoka katika sanamu la Yesu Mtoto liitwalo Niñopa, katika Kanisa la Parokia ya Manispaa ya Xochimilco ('Sochimiliko') la Iglesia de San Bernardino de Siena, Mexico City, kulikuwa na nyumba ndogo ya siri ('safe house') ya Kolonia Santita iliyojengwa bila uzio wa ukuta au seng’enge isipokuwa miti iliyopandwa kuizunguka bila mpangilio wowote. Ndani ya nyumba hiyo Mpelelezi Maarufu Duniani John Murphy alikuwa akiteswa na magaidi kumi na mbili; waliokuwa wakiendelea kushangaa jinsi alivyookoka katika ajali ya ndege iliyoua watu zaidi ya mia tatu huko Uholanzi, na jinsi alivyoweza kuingia katika ofisi ya siri ya Panthera Tigrisi, kitu kilichomchanganya akili Tigrisi na makompade wote wa Kolonia Santita duniani kote. Bila Mtoto wa Rais wa Meksiko Debbie Patrocinio Abrego, na mwanasesere wa nyoka wa Mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Lisa Madrazo Graciano, John Murphy angeanguka.”
Enock Maregesi