Debbie Patrocinio Abrego Quotes
Quotes tagged as "debbie-patrocinio-abrego"
Showing 1-12 of 12

“Usiwe na wasiwasi, Peter. Hizo ni hisia zangu tu. Huwezi kuwa mpelelezi. Lakini, kusema ule ukweli, ningependa sana kuonana na John Murphy. Kuna kazi binafsi ningependa kumpa. Wewe unatoka Afrika, hujawahi kumwona?â€� Debbie alizidi kumshtua Murphy.
“Nani?� Murphy aliuliza huku akitabasamu.
“John Murphy wa Afrika.�
“Sijawahi kumwona. Mbona unamuulizia hivyo?�
Debbie alitulia. Kisha akarusha nywele ili aone vizuri.
“Nampenda sana!�
“Kwa nini?�
“Simpendi kwa mahaba, lakini.�
“Ndiyo. Kwa nini?�
“OK. Nampenda kwa kipaji chake. Alichopewa na Mungu, cha ujasusi. Kusaidia watu.�
“Ahaa!� Murphy alidakia, sasa akifikiri sana.
“Murphy ana mashabiki wengi hapa Meksiko bila yeye mwenyewe kujua, kwa sababu ya kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya � hasa wa huku Latino. Tatizo lake haonekani. Wengi hudhani ni hadithi tu, kwamba hakuna mtu kama huyo hapa duniani.�
“Hapana! Murphy yupo! Ni mfanyabiashara maarufu huko Tanzania. Lakini ndiyo hivyo kama unavyosema ... Haonekani!”
― Kolonia Santita

“Mpenzi. Sikiliza. Magaidi yaliyomuua Marciano yana mtandao dunia nzima na watu wote wanayajua. Yanaitwa Kolonia Santita. Tatizo hata hivyo ni moja: Hakuna mtu amewahi kuthibitisha au kutoa ushuhuda wa uhalifu wao ili watiwe nguvuni. Huendesha maisha yao kibabe na yana kila mbinu ya kukwepa sheria, ndani na nje ya Meksiko. Watu wengi wameuwawa kwa sababu ya Kolonia Santita. Ukileta kidomodomo yanakuua; au yanakupa notisi ya kuhama mji au nchi, ukakae mbali na Meksiko au Mexico City.”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Majambazi huwapenda wanaowapenda. Chukulia mfano huu: Mimi na Wanda ni marafiki, OK? Baba yake, au genge la baba yake, hataweza kunidhuru au kuwadhuru watu ninaowapenda kwa sababu tu ya urafiki na mtoto wake. Na yeye anaweza kufumbiwa macho akifanya makosa kwa sababu mimi na mtoto wake ni marafiki wakubwa. Murphy, hapa Meksiko tuna kitu kinaitwa Bima ya Utekaji Nyara ('Ransom Insurance'). Zamani nilikuwa nalipa dola milioni kumi za Marekani kama bima ya utekaji nyara; Lisa alikuwa analipa milioni nne na Wanda bado analipa milioni mbili mpaka sasa hivi. Baada ya mimi na Lisa kujenga urafiki na Wanda, malipo yetu ya bima yamepungua mpaka dola milioni moja kwa mwaka.”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Peter, naomba nitubu kosa. Mimi si mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ni mtoto wa Rais wa Meksiko. Lisa ni mtoto wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,â€� Debbie alisema akitabasamu.
“Hata mimi nilijua ulikuwa ukinidanganya. Lakini mbona Rais wa Meksiko haitwi Patrocinio Abrego?� Murphy aliuliza.
“Utamaduni wa Meksiko ni tofauti kidogo na tamaduni zingine,â€� Debbie alijibu baada ya kurusha nywele nyuma kuona vizuri. “Hapa, watu wengi hawatumii majina ya pili ya baba zao. Hutumia jina la kwanza la mama la pili la baba; ndiyo maana Wameksiko wengi wana majina matatu. Kwa upande wangu, Patrocinio ni jina la baba yake mama yangu na Abrego ni jina la babu yake mama yangu â€� kwa sababu za kiusalama.”

“Murphy. Sina mbinu zozote za kujikinga kama unavyojua; mbali na mafunzo ya FBI. Baada ya kumrusha nyoka wa Lisa nywele zilinisisimka. Wazo la kukimbia likaja ghafla. Kukimbia hata hivyo nikashindwa kwa kuhofu huenda wangeniona. Hivyo, nikarudi nyuma ya nyumba na kupanda mti na kujificha huko. Bunduki zilipolia, nilijua wamekuua. Ila kitu kimoja kikanishangaza: mashambulizi hayakuonekana kukoma. Kitu hicho kikanipa nguvu kwamba huenda hujafa na ulikuwa ukipambana nao. Kimya kilipotokea nilijua umewashinda nguvu, kitu ambacho kumbe kilikuwa kweli. Nilipokutafuta baadaye lakini bila kukuona kutokana na kukurukakara za maadui niliamua kwenda katika gari ili nije na gari kama mgeni, nikitegemea waniruhusu kuingia ili nipate hakika kama wamekuua au bado uko hai. Wasingenifanya chochote. Kimaajabu, niliposhuka katika mti ili nikimbie katika gari, niliona gari ikija kwa kasi. Kuangalia vizuri nikakuta ni Ferrari, halafu nikashangaa nani anaendesha gari ya Lisa!â€�
Murphy alitabasamu tena na kuendelea kusikiliza.
“Sijui moyo wangu ulikuwaje. Sikuogopa tena! Badala yake nilikaza mwendo na kuendelea kuifuata huku nikipata wazo hapohapo kwamba mtu aliyekuwemo akiendesha hakuwa adui. Adui angeingia katika gari na kunisubiri aniteke nyara.� Debbie alitulia.
“Ulihisi ni mimi?� Murphy aliuliza.
“Nilihisi ni mtu tu mwema amekuja kunisaidia ... au mwizi wa gari. Hata hivyo, baadaye nilijua ni wewe na furaha yangu yote ilirudi.”

“Nusu dakika baada ya kuondoa gari, Murphy aliona kiwiliwili cha mtu kikimwendea mbio kutokea katika nyumba ya magaidi! Hapohapo alisimamisha gari na kuacha taa zikiwaka, halafu akashika bunduki na kushuka â€� akiwa ameangalia mbele kwa tahadhari kubwa. Alikuwa mwanamke. Debbie! Murphy alipojua ni Debbie, alitupa bunduki na kuchomoka mbio mpaka wakakutana na kukumbatiana kwa nguvu! Murphy alimbeba Debbie na kumbusu kila sehemu, halafu akamfuta machozi na kumbembeleza.”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Kesho yake Ijumaa Rais wa Meksiko alirudi kutoka Panama na aliomba kuonana na Vijana wa Tume; alitaka kuwapongeza binafsi, na kuwapa nishani za heshima kwa mchango wao mkubwa kwa Jamii ya Meksiko. Randall Ortega alilipeleka ombi hilo kwa Rais wa Tume ya Dunia; Rais wa Tume ya Dunia akakaa na Kamati ya Usalama ya Tume ya Dunia na kumrudishia Randall Ortega jawabu, kwamba Vijana wa Tume waliruhusiwa kuonana na Rais wa Meksiko na baadhi ya maafisa wa juu wa serikali ya shirikisho. Saa mbili usiku wa siku hiyo, Ijumaa, kulifanyika sherehe ndogo ya siri nyumbani kwao Debbie; sherehe iliyohudhuriwa na Rais wa Meksiko na mke wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Meksiko, Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya Nchini Marekani, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu Nchini Meksiko, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, maafisa wa tume na watu wengine wa muhimu katika kazi ya Vijana wa Tume.”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Sigara zilizidi kuvutwa, ndani ya nyumba, na magaidi wale wawili, wakati Murphy akisinzia kudanganyia kama kweli nguvu zilishamwisha. Alimfikiria tena mpenzi wake Sophia, safari hii sana. Alimkumbuka Debbie; hakujua alikuwa wapi na hakujua mama yake angefanya nini kama Debbie angekufa, na Murphy ndiye aliyetoka naye. Debbie alimuuma zaidi. Alimkataza kufa kwa ajili ya mchumba wake. Sasa alikufa kwa ajili ya mtu ambaye hakumjua. Murphy alijilaumu kumtongoza na kumchukua kwao na kulala naye na kula chakula chake cha kifalme. Wazazi wake wangejisikiaje kama angekufa, tena katika mazingira ya kutatanisha kama yale. Kufa alijua angekufa; lakini Mungu angemsaidia, awaage watu wake.”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Ndani ya chumba, akiwa bado amechanganyikiwa, akiwa hajui Debbie alikokwenda, Murphy alisikia walinzi wakipiga kelele nje. Kamanda huwa anakuwa shetani nyakati kama hizo. Alibeba pumzi. Mikononi mwake akiwa na M-16, Debbie kichwani; Murphy alishangaza umati wa watu! Risasi zaidi ya sitini zilifyatuka katika bunduki, mlango wote ukabomoka â€� ndani ya sekunde kumi!”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Wakati Ford Bronco inatoka katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals S.A de C.V. (kilichomilikiwa na mkurugenzi mkuu wa 'methamphetamine' wa Kolonia Santita mfanyabiashara wa Kichina kutoka Chaling, katika jimbo la Hunan, kusini ya kati ya China, Li Dongyang; na mkurugenzi wa usalama wa Kolonia Santita kutoka Lomas de Chapultepec, Mexico City, Gortari Manuel) Daniel Yehuda na Radia Hosni, waliokuwa wakipiga picha kila kitu kilichokuwa kikiingia na kutoka kiwandani kwa ajili ya ripoti ya upelelezi wao ya baadaye, waliiona. Lakini, hawakujua kama ilikuwa ikienda Varsovia kumuua Murphy na Sajini Mogens.
Bronco ilipofika Varsovia ilisimama kwa fujo mbele ya SUV ya msafara wa Mtoto wa Rais Debbie Patrocinio Abrego, aliyekuwa ndani ya Mgahawa wa Angus akicheza muziki wa 'mariachi' na John Murphy, huku Mogens akilinda usalama wa kamanda wake na usalama wa baa nzima. Kabla majambazi wa Kolonia Santita hawajaleta madhara au fujo yoyote kwa Vijana wa Tume, polisi walifika eneo lile haraka ilivyowezekana! Kwa msaada wa walinzi wa Debbie! Wale majambazi walipekuliwa na kukutwa na bastola moja ya Akdal Ghost, bunduki mbili za AK-47, na picha nne za Vijana wa Tume ndani ya gari yao. Polisi waliwakamata na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Tume ya Dunia kilichopo Zona Rosa, Mexico City.”
―

“Kilometa mbili na ushei kidogo kutoka katika sanamu la Yesu Mtoto liitwalo Niñopa, katika Kanisa la Parokia ya Manispaa ya Xochimilco ('Sochimiliko') la Iglesia de San Bernardino de Siena, Mexico City, kulikuwa na nyumba ndogo ya siri ('safe house') ya Kolonia Santita iliyojengwa bila uzio wa ukuta au seng’enge isipokuwa miti iliyopandwa kuizunguka bila mpangilio wowote. Ndani ya nyumba hiyo Mpelelezi Maarufu Duniani John Murphy alikuwa akiteswa na magaidi kumi na mbili; waliokuwa wakiendelea kushangaa jinsi alivyookoka katika ajali ya ndege iliyoua watu zaidi ya mia tatu huko Uholanzi, na jinsi alivyoweza kuingia katika ofisi ya siri ya Panthera Tigrisi, kitu kilichomchanganya akili Tigrisi na makompade wote wa Kolonia Santita duniani kote. Bila Mtoto wa Rais wa Meksiko Debbie Patrocinio Abrego, na mwanasesere wa nyoka wa Mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Lisa Madrazo Graciano, John Murphy angeanguka.”
―
―
All Quotes
|
My Quotes
|
Add A Quote
Browse By Tag
- Love Quotes 99.5k
- Life Quotes 78k
- Inspirational Quotes 74.5k
- Humor Quotes 44.5k
- Philosophy Quotes 30.5k
- Inspirational Quotes Quotes 27.5k
- God Quotes 26.5k
- Truth Quotes 24.5k
- Wisdom Quotes 24k
- Romance Quotes 24k
- Poetry Quotes 23k
- Life Lessons Quotes 21k
- Death Quotes 20.5k
- Quotes Quotes 19k
- Happiness Quotes 19k
- Hope Quotes 18k
- Faith Quotes 18k
- Inspiration Quotes 17k
- Spirituality Quotes 15.5k
- Religion Quotes 15k
- Motivational Quotes 15k
- Writing Quotes 15k
- Relationships Quotes 15k
- Life Quotes Quotes 14.5k
- Love Quotes Quotes 14.5k
- Success Quotes 13.5k
- Time Quotes 12.5k
- Motivation Quotes 12.5k
- Science Quotes 12k
- Motivational Quotes Quotes 11.5k