Å·±¦ÓéÀÖ

Alamu Quotes

Quotes tagged as "alamu" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Kutokana na utafiti wa kisayansi wa kionairolojia ambayo ni sayansi ya ndoto; wakati tumelala, sehemu yetu ya akili isiyotambua huamka na kuanza kazi; kwa kupangilia mawazo, kuanzia mawazo ya siku iliyopita, na kuimarisha mahusiano baina ya mawazo hayo na matukio ya wakati ujao, huku ikiondoa mawazo yasiyokuwa na maana, kunusuru ubongo usielemewe na msongo. Kazi hiyo hutambuliwa haraka na akili inayotambua, kwa njia ya alamu, lakini akili inayotambua inapagawa kwa sababu haijui akili isiyotambua inamaanisha nini kutuma alamu kama hizo. Kwa hiyo inajaribu kwa kadiri inavyoweza kutunga hadithi kuhusiana na vitu mbalimbali, ambayo baadaye hutafsiriwa kama ndoto. Hii ndiyo sababu tunaota ndoto za ajabu ambazo aghalabu hazina maana yoyote, na hazina maana yoyote kwa sababu hazitakiwi kuwa na maana yoyote, na hazina ujumbe wowote halisi kutoka akilini mwetu. Hayo ni matokeo ya akili kujaribu kusanisi sauti, kutoka katika akili isiyotambua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mapenzi, kama ilivyo kwa vitu vyote hapa ulimwenguni, hayawezi kuwepo bila kujumuishwa na fizikia na kemia yake! Bila kemia hakuna mapenzi ya kudumu. Tamaa ya ngono kimsingi huanza pindi unapokutana na mtu. Tamaa hiyo huweza kukua na kuwa kitu kingine kadiri muda unavyokwenda lakini chanzo kinakuwepo toka siku ya kwanza mlipokutana. Kemikali inayosababisha tamaa ya ngono na hata kuikuza tamaa hiyo ni 'phenyl ethylamine' ('fino itholamine') au PEA ambayo ni kemikali ya mapenzi ndani ya ubongo. Husisimua watu na huongeza nguvu za kimwili (fizikia) na kihisia (kemia). Tamaa husababisha mtu azalishe PEA nyingi zaidi, kitu kinachosababisha kujisikia kizunguzungu (cha hisia za kimapenzi) na dalili zingine kama magoti kutetemeka, jasho kutoka viganjani na kutokutulia. Kemikali hii inapozalishwa kwa kiwango kikubwa, hutuma alamu ('signals') kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye viungo vingine vya mwili na kutumika kama 'dopamine' au 'amphetamine' ambazo ni kemikali za ulevi ndani ya ubongo. Iwapo unajiuliza kwa nini wewe au mtu mwingine unavutiwa na mtu ambaye hamwendani kimapenzi, inaweza kuwa ni kwa sababu una kiwango kikubwa cha kemikali hizo kuliko mwenzako, kitu ambacho huzidi uwezo wa kutumia kichwa na kutoa maamuzi bora kulingana na akili ya kuzaliwa.

Kwa jumla, mapenzi yote ya kweli uhitaji angalau kiwango kidogo cha PEA kwa wale wanaopendana. Cha msingi kukumbuka ni kwamba kemikali hizi huja kwa vituo, nikiwa simaanishi kwamba tamaa ya ngono hupotea pale mtu anapoelekea kwenye uhusiano wa kudumu. Lakini mambo hubadilika. Hatuwezi kuvumilia zile hisia kali kadiri tunavyozidi kusafiri kuelekea kwenye uhusiano wa kudumu na kwenye maisha ya pamoja yenye furaha. Katika uhusiano wenye afya hata hivyo matatizo hutokea hapa na pale. Chanzo cha Murphy na Debbie kupendana kilikuwa kemia zaidi kuliko fizikia. Kama hakuna kemia hakuna mapenzi.”
Enock Maregesi