欧宝娱乐

Huzuni Quotes

Quotes tagged as "huzuni" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Marafiki wanaweza kukupotosha bila wao wenyewe kujua na bila kuwa na nia mbaya ya aina yoyote ile; na wanaweza kuwa washauri wazuri kwa sababu wanakujua vizuri unapokuwa na huzuni, na wanakujua vizuri unapokuwa na furaha pia. Kwa mfano; rafiki yako anaweza kukushauri kusomea uhasibu wakati Mungu amekupangia utawala, au anaweza kujua aongee na wewe wakati gani kulingana na tabia yako ya kubadilikabadilika. Maadui wanasaidia kujua kipaji ulichopewa na Mungu 鈥� ukifanya kitu ambacho si cha kawaida katika maisha yako halafu ukawa na maadui ujue hicho ndicho Mungu alichokupangia kufanya, hivyo usikate tamaa 鈥� na mashabiki wanasaidia kufanya kipaji chako kiwe na uhai.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Aidha, tunaweza kupata inkishafi kutokana na asili ya miili yetu, matukio fulani ya wakati ujao yana asili yake katika ndoto za binadamu. Ndoto hizo au maono hayo ni ishara ya kile kinachokuja mbele katika maisha ya mtu; kama vile afya, ugonjwa au hatari. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira 鈥� unatakiwa kuwa na hekima; ukiota kuhusu mimba na unajifungua, hiyo ni ishara ya kuwa katika mchakato wa kutengeneza wazo jipya 鈥� unatakiwa kushukuru; ukiota unaruka angani, hiyo ni ishara ya tumaini 鈥� unatakiwa kushukuru; ukiota kuhusu maji au kiowevu kingine chochote kile, hiyo ni ishara ya siri na wakati mwingine ni ishara ya kuwa na matatizo ya kiafya kama utaota kuhusu maji machafu 鈥� unatakiwa kuwa msiri na msafi; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni 鈥� unatakiwa kuomba; na ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio 鈥� unatakiwa kushukuru.”
Enock Maregesi