Å·±¦ÓéÀÖ

Hasira Quotes

Quotes tagged as "hasira" Showing 1-14 of 14
Enock Maregesi
“Hasira ni Shetani. Hekima ni Mungu. Kila kitu kimo ndani yetu. Hasira imo ndani yetu. Hekima imo ndani yetu. Atomu ni matofali ya ujenzi wa kila kitu ulimwenguni likiwemo jua na miili ya wanadamu. Ndani ya atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi. Kama miili yetu imetengenezwa na atomu na katika kila atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi, hivyo basi, tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mazuri na tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mabaya. Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana. Geuza hasira yako kuwa hekima kwa faida yako na kwa faida ya wengine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Geuza hasira yako kuwa hekima.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kinachotokea katika dunia hii si kitu kizuri cha kuzoea au hata kufikiria. Hivyo tuna haki ya kuwa na mawazo, hasira na wanyonge kuhusiana na suala zima la maisha yetu hapa duniani. Hata hivyo hali hii itabaki kuwa hivyo kwa sababu Mungu ametaka iwe hivyo kwa sasa. Kwa maana hiyo, hekima ni kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Lazima tukubaliane na kisichoweza kufikirika kuweza kubadilika.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mammon ni mungu wa pesa wa kuzimu anayesimamia mambo yote ya kifedha ulimwenguni. Ni miongoni mwa mashetani saba waliotupwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kutokea mbinguni akiwemo Ibilisi, Beelzebub, Asmodeus, Leviathan, Amon na Belphegor. Ibilisi ni mungu wa kiburi, Beelzebub ni mungu wa uroho, Asmodeus ni mungu wa zinaa, Leviathan ni mungu wa wivu, Amon ni mungu wa hasira na Belphegor ni mungu wa uvivu. Jukumu la mashetani hawa ni kusimamia kwa uaminifu mkubwa kutokea kuzimu dhambi kubwa saba duniani ambazo ni kiburi, uroho, zinaa, wivu, hasira, uvivu na uchoyo. Dawa ya dhambi hizo ni busara, kiasi, ujasiri, imani, haki, tumaini na upendo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi wanamwabudu Shetani. Lakini Shetani wanayemwabudu si Shetani Ibilisi aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu kuja kuudanganya ulimwengu wote. Ni Shetani roho ya mabadiliko, mabadiliko ya kweli, ya ufahamu kamilia ulimwengu huu ambamo sisi sote tunaishi. Wachawi, kwa maneno mengine, wanaabudu miungu â€� kama vile Inanna wa Mesopotamia, Isis wa Misri, Asherah wa Kaanani au Belus wa Assyria ambaye ndiye mungu wa kwanza kuabuadiwa kama sanamu duniani â€� iliyotwaliwa na Shetani tangu misingi ya ulimwengu huu kusimikwa. Dhambi aliyotenda Shetani mbinguni ni ndogo kuliko dhambi wanazotenda wachawi duniani, ijapokuwa dhambi aliyotenda Shetani haitaweza kusamehewa na ndiyo maana Shetani hataweza kuwasamehe wanadamu. Ni jukumu letu kuwaita wachawi wote kutoka Babeli na kuwaleta katika ukweli kama kweli wanayemwabudu ni Shetani Ibilisi, Shetani Beelzebub, Shetani Asmodeus, Shetani Leviathan, Shetani Mammon, Shetani Amon au Shetani Belphegor ambao ni mabingwa wa kiburi, uroho, zinaa, wivu, fedha, hasira na uvivu duniani. Wachawi hawajui, na usipojua waweza kufa bila kujua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Aidha, tunaweza kupata inkishafi kutokana na asili ya miili yetu, matukio fulani ya wakati ujao yana asili yake katika ndoto za binadamu. Ndoto hizo au maono hayo ni ishara ya kile kinachokuja mbele katika maisha ya mtu; kama vile afya, ugonjwa au hatari. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira â€� unatakiwa kuwa na hekima; ukiota kuhusu mimba na unajifungua, hiyo ni ishara ya kuwa katika mchakato wa kutengeneza wazo jipya â€� unatakiwa kushukuru; ukiota unaruka angani, hiyo ni ishara ya tumaini â€� unatakiwa kushukuru; ukiota kuhusu maji au kiowevu kingine chochote kile, hiyo ni ishara ya siri na wakati mwingine ni ishara ya kuwa na matatizo ya kiafya kama utaota kuhusu maji machafu â€� unatakiwa kuwa msiri na msafi; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni â€� unatakiwa kuomba; na ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio â€� unatakiwa kushukuru.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanawake wenye umri wa miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili wanaweza kutawaliwa. Ishirini na mbili hadi ishirini na nne wanaweza kukuumiza. Ishirini na nne hadi ishirini na saba unaweza kuweka malengo nao yenye natija. Ishirini na saba hadi thelathini watakuchunguza sana na hawatakupenda kutoka moyoni. Thelathini hadi thelathini na tano wamejawa na dharau za kijinga. Thelathini na tano hadi arobaini na mbili watakung’ang’ania kupoza hasira za huko walikotoka. Tofauti na wanawake wenye umri wa miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili, na wanawake wenye umri wa miaka ishirini na nne hadi ishirini na saba, wengine wote ni kubahatisha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukikasirika, aliyesababisha ukasirike ni Shetani aliyeko ndani yako; na ukiwa na furaha, aliyesababisha uwe na furaha ni Mungu aliyeko ndani yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Geuza hasira yako kuwa hasira ya Mungu ya haki.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shinda hasira ndani ya moyo wako kwa silaha ya furaha.”
Enock Maregesi