欧宝娱乐

Jumatano Quotes

Quotes tagged as "jumatano" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Meja Jenerali U Nanda, 60, Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, alizaliwa Jumamosi ya tarehe 19/03/1932 kandokando ya mto huko Maubin nchini Bama. Yeye na familia yake ni waumini wa dini ya Ubuda. Mke wake, Daw Aung Phyu, ana miaka 57. Alizaliwa Jumapili ya tarehe 20/10/1935. Nanda na Aung Phyu wana watoto watatu. Ko Mahn Thiri (wa kiume na wa kwanza kuzaliwa) ana miaka 37. Alizaliwa Alhamisi ya tarehe 08/12/1955. Yeye na familia yake wanakaa nchini Tailandi. Ma Nang Nyi ni mtoto wa pili wa familia ya Nanda na Aung Phyu. Alikufa kwa madawa ya kulevya Jumamosi ya tarehe 12/05/1980 akiwa na miaka 23. Alizaliwa Jumamosi ya tarehe 06/04/1957. Miaka miwili baadaye mpenzi wake wa kiume, Ko San Pe, alikufa kwa madawa ya kulevya pia Jumatano ya tarehe 21/07/1982 akiwa na miaka 25. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 29/01/1957. Ma Thida Wai Aung ni wa mwisho kuzaliwa. Ana miaka 34. Alizaliwa Jumatano ya tarehe 23/07/1958. Anakaa Rangoon na mume wake wa miaka sita na watoto wawili, wa kike na wa kiume. Saw Saya (Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, kutoka katika kabila la Karen) ndiye aliyempa taarifa U Nanda za kikao cha dharura cha Tume ya Dunia. Ana miaka 54. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 01/03/1938.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu Kristo hakufa siku ya Ijumaa jioni na kufufuka siku ya Jumapili asubuhi. Alikufa siku ya Jumatano jioni na kukufuka siku ya Jumamosi jioni. Wakati kifo kinamkumba, hakuwa na umri wa miaka 33, alikuwa na umri wa miaka 31. Kama Yesu Kristo alikufa siku ya Ijumaa jioni, na kufufuka siku ya Jumapili asubuhi, hatuna Mwokozi!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu Kristo wa Nazarethi ni mtu mashuhuri zaidi kuliko wote kuwahi kukanyaga ardhi ya dunia hii. Alikufa majira ya saa 9 kamili za mchana, siku ya Jumatano, katika kipindi cha demani cha AD 31. Saa chache baadaye, jua lilipokuwa likizama, alilazwa katika kaburi jipya la Yusufu wa Arimathaya. Katika siku ya kawaida ya Sabato, Jumamosi, siku tatu kamili baada ya mazishi yake, Mungu Baba alimfufua Mtoto Wake kwa ajili ya uzima wa milele.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hii ni muhimu sana kwa Pasaka. Si tu kwamba Pasaka ni tamasha linalojitegemea, lakini kadhalika linatumika kama siku ya maandalizi kwa ajili ya siku takatifu, siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mkate Usiotiwa Chachu. Kwa mujibu wa hesabu za kalenda ya Kihebrania, Pasaka inaweza kuangukia siku ya Jumatatu, Jumatano, Ijumaa au Sabato.”
Enock Maregesi