欧宝娱乐

Dini Quotes

Quotes tagged as "dini" Showing 1-7 of 7
Enock Maregesi
“Meja Jenerali U Nanda, 60, Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, alizaliwa Jumamosi ya tarehe 19/03/1932 kandokando ya mto huko Maubin nchini Bama. Yeye na familia yake ni waumini wa dini ya Ubuda. Mke wake, Daw Aung Phyu, ana miaka 57. Alizaliwa Jumapili ya tarehe 20/10/1935. Nanda na Aung Phyu wana watoto watatu. Ko Mahn Thiri (wa kiume na wa kwanza kuzaliwa) ana miaka 37. Alizaliwa Alhamisi ya tarehe 08/12/1955. Yeye na familia yake wanakaa nchini Tailandi. Ma Nang Nyi ni mtoto wa pili wa familia ya Nanda na Aung Phyu. Alikufa kwa madawa ya kulevya Jumamosi ya tarehe 12/05/1980 akiwa na miaka 23. Alizaliwa Jumamosi ya tarehe 06/04/1957. Miaka miwili baadaye mpenzi wake wa kiume, Ko San Pe, alikufa kwa madawa ya kulevya pia Jumatano ya tarehe 21/07/1982 akiwa na miaka 25. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 29/01/1957. Ma Thida Wai Aung ni wa mwisho kuzaliwa. Ana miaka 34. Alizaliwa Jumatano ya tarehe 23/07/1958. Anakaa Rangoon na mume wake wa miaka sita na watoto wawili, wa kike na wa kiume. Saw Saya (Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, kutoka katika kabila la Karen) ndiye aliyempa taarifa U Nanda za kikao cha dharura cha Tume ya Dunia. Ana miaka 54. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 01/03/1938.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu alilibariki taifa la Israeli katika misingi ya kidini na si katika misingi ya kisiasa au misingi ya kihistoria; na asili ya dini ya Kikristo ni kutoka katika taifa hilo ambalo Biblia imelitaja kama taifa teule la Mwenyezi Mungu. Mgogoro wa Israeli na Palestina ulianzishwa na Israeli mwenyewe. Yakobo alipokea baraka iliyokuwa si ya kwake kwa kutumia hila ya Rebeka. Baraka ya Yakobo ilikuwa ya Esau.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukanda wa Gaza ni jimbo lenye miji minne na kambi mbalimbali za wakimbizi za Umoja wa Mataifa 鈥� lenye urefu wa kati ya kilometa 41 au maili 25 na lenye upana wa kati ya kilometa 6 mpaka 12 au maili 3.7 mpaka 7.5, pamoja na eneo la jumla la kilometa za mraba 365 au maili za mraba 141. Jimbo hili liliwahi kutawaliwa na Wamisri, Wakaanani, Waisraeli, Wasiria, Wababelonia, Wagiriki, Warumi, Waturuki, Waingereza, na Wapalestina, na limekuwa uwanja wa vita kwa karne nyingi kwa sababu za kidini na kihistoria. Ukanda wa Gaza uko chini ya Palestina. Uko chini ya serikali ya Hamas.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuwa mkristo wa kanisa au wa dini ni kughushi imani 鈥� na kughushi imani ni dhambi kubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ana mpango na maisha ya kila mtu hapa duniani bila kujali dini, jinsia, kabila, rangi, taifa, au umri, na kila mtu ni wa kipekee.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Bila kujali dini ya mtu, bila kujali anaamini nini, kila mtu anatakiwa kujua kusudi la maisha yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukimpigia mtu kura kwa sababu za kishabiki, kikabila, kidini, kirafiki au rushwa, umeshindwa kuongea na nchi yako kama inavyopaswa, umeshindwa kuwa mzalendo wa kweli, usimlalamikie yule aliyechaguliwa.”
Enock Maregesi