欧宝娱乐

Lengo Quotes

Quotes tagged as "lengo" Showing 1-6 of 6
Enock Maregesi
“Lengo kuu la Kolonia Santita kuuza madawa hayo ni kuwafadhili askari wa msituni wa Kolombia (magorila wa vyama visivyokuwa rasmi vya kisiasa au vyama haramu vya kisiasa) kushika hatamu za uongozi wa Kolombia, kwa makubaliano ya Kolonia Santita kutawala biashara ya kokeini ya taifa hilo la Amerika ya Kusini. WODEA lazima ilizuie Shirika la Madawa ya Kulevya la Kolonia Santita kuuza madawa hayo kwa gharama yoyote ile, pesa au damu, kutetea afya na amani ya dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu alikupa vipaji ili uwanufaishe wengine na si kujinufaisha mwenyewe, na aliwapa wengine vipaji ili kukunufaisha wewe na si kujinufaisha wenyewe, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika dunia yetu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mimi ni mwana wa Mungu. Sisi sote ni watoto wa Mungu. Lengo la kuzaliwa kwangu ni kufanya kazi pamoja na Roho Mtakatifu na malaika kumtumikia Bwana, na kueneza injili ya Yesu Kristo duniani kote, kupitia vitabu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Katika umoja hakuna 'umimi', kuna 'sisi kwa pamoja'; na lengo la umoja ni kutengeneza nguvu, ya ziada.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Njia rahisi ya kujua maana ya ndoto zako ni kurekodi ndoto zako kila siku asubuhi, au kila unapoota, kwa angalau majuma mawili. Baada ya muda huo ndoto zako zitaanza kuleta maana. Lengo lake kubwa ni kukufanya ujitambue.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani lengo lake ni kutawala dunia. Huwezi kutawala dunia bila elimu!”
Enock Maregesi