Å·±¦ÓéÀÖ

Madawa Quotes

Quotes tagged as "madawa" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Lengo kuu la Kolonia Santita kuuza madawa hayo ni kuwafadhili askari wa msituni wa Kolombia (magorila wa vyama visivyokuwa rasmi vya kisiasa au vyama haramu vya kisiasa) kushika hatamu za uongozi wa Kolombia, kwa makubaliano ya Kolonia Santita kutawala biashara ya kokeini ya taifa hilo la Amerika ya Kusini. WODEA lazima ilizuie Shirika la Madawa ya Kulevya la Kolonia Santita kuuza madawa hayo kwa gharama yoyote ile, pesa au damu, kutetea afya na amani ya dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wakiwa na suti nzito za kijani na madoa meusi (‘Ghillie Suitsâ€�) kwa ajili ya kupigania porini; Vijana wa Tume walikuwa na kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (iliyokuwa na uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migongoni mwao juu ya vizibao vya kuzuia risasi, vitibegi vya msalaba mwekundu (‘Blowout Kitsâ€� â€� katika mapaja ya miguu yao ya kulia, ndani yake kukiwa na pisto na madawa ya huduma ya kwanza), vitibegi vya kujiokolea (‘Evasion Kitsâ€� â€� katika mapaja ya miguu yao ya kushoto, ndani yake kukiwa na visu na pesa na ramani ya Meksiko) na bunduki za masafa marefu. Kadhalika, Vijana wa Tume waliamua kuchukua Punisher â€� waliyoafikiana baadaye kuwa ilikuwa nzuri kuliko RPG-7, ‘Rocket Propelling Gunâ€�, ambayo Mogens alipendekeza waitumie kubomolea Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals; kwa sababu hakutaka kuleta madhara kwa watu waliokuwa hawana hatia.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kujua ukweli juu ya uraibu wa madawa ya kulevya kunaweza kumsaidia mtu kujua madhara ya madawa ya kulevya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ili kupambana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika jamii ya Tanzania, ni muhimu kutoa elimu kwa Watanzania juu ya madhara yanayoambatana na matumizi ya madawa hayo. Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya kulevya pia.”
Enock Maregesi