Å·±¦ÓéÀÖ

Maadili Quotes

Quotes tagged as "maadili" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Hasanati ni matendo mema. Mema yanatoka kwa Mungu. Mabaya yanatoka kwa Shetani. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Mke mbaya anatoka kwa Shetani. Mke mwema ana hekima na busara, ana maadili na tabia njema, ana utu na uchapakazi, ana wema na upendo, na ana aibu kwa wanaume.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Radia hakuwa na makosa. Wengi huishi maisha yao bure. Yeye aliishi ya kwake kwa ajili ya watu. Hakuishi tu kama raia wa Tunisia. Aliishi kama raia wa uanadamu, maadili mema na uchapakazi. Watu walimsifu kwa kuwa na kaulimbiu ya 'Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta'.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kila mtu ana tabia, matendo, mawazo na akili yake tofauti na mtu mwingine hapa duniani. Usimdharau mtu ukidhani ana akili kama za kwako au anafikiri kama unavyofikiri wewe kwani kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Unaweza kudhani unamjua mtu kumbe humjui. Heshimu kila mtu kama unavyojiheshimu kwa sababu, kila mtu ni wa pekee. Kama tunavyotofautiana katika vidole na macho ndivyo tunavyotofautiana katika tabia, matendo, mawazo, imani, maadili na akili. Usimdharau mtu usiyemjua au unayedhani unamjua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sababu ya kupanda na kuanguka kwa mataifa ni ya kimaadili na kiroho. Hakuna taifa linaloweza kutegemea nguvu na mali zake ili kujiokoa kutokana na madhara ya ukiukwaji wa maadili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tajiri bila maskini ni maskini na bila tajiri maskini ni tajiri. Tajiri akiwa na maadili, maskini atakuwa tajiri.”
Enock Maregesi