Å·±¦ÓéÀÖ

Maamuzi Quotes

Quotes tagged as "maamuzi" Showing 1-8 of 8
Enock Maregesi
“Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali mara nyingi hutegemea ujasusi wa ndani na nje kufanya maamuzi mazito na sahihi ya kuendesha nchi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake yote. Fanya kile ulichosema utafanya, hata kama sehemu ya kile ulichosema utafanya uliinukuu kutoka kwa wengine, hata kama watu hawatakubaliana na wewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ina thamani pale unapokuwa nayo, si pale unapokuwa huna, hivyo iweke mahali unapoweza kuiona: katika nyumba, katika shamba au katika elimu. Badala ya kumpa mtu pesa ili ajenge nyumba, mpe nyumba. Badala ya kumpa mtu pesa ili afanye biashara, mpe biashara. Halafu, mpe elimu afanye maamuzi ya biashara yake. Pesa ina laana na Mungu pekee ndiye anayeweza kuiondoa laana hiyo. Ni rahisi kwa tajiri kupata baraka ya pesa kwa sababu ana pesa na ana uwezo mkubwa wa kusaidia maskini. Ni vigumu kwa maskini kupata baraka ya pesa kwa sababu hana au ana uwezo mdogo wa kusaidia maskini. Mungu anaweza kuondoa laana ya pesa kupitia hisani kwa maskini, kitu ambacho aghalabu hufanywa na matajiri wenye uwezo mkubwa. Heri kutoa kitu au huduma au elimu kwa maskini kuliko pesa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tunapaswa kuyafikiria madhaifu yetu na dhambi zetu kwa makini sana, kwa kiasi cha kuyashinda madhaifu hayo na dhambi hizo, kabla hatujatoa maamuzi makali dhidi ya wenzetu. Tunawezaje kumlaumu mtu wakati hata sisi wenyewe tunaweza kuwa na matatizo makubwa? Tusiwe wanafiki. Badala ya kulaumu, saidia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usilaumu, usilipize kisasi, usilaani, usihukumu, wala usitoe adhabu, lakini kuwa makini sana na maamuzi yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali haishirikiani na huruma katika kufanya maamuzi yake. Inashirikiana na akili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tume ya uchaguzi ikiidhinisha matokeo halafu watu wakalumbana hayo ni matatizo yenu. Nchi imeshatoa maamuzi yake.”
Enock Maregesi