Adamu Quotes
Quotes tagged as "adamu"
Showing 1-9 of 9

“Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu.”
―
―

“Shetani alikuwa malaika aliyeumbwa na Mungu lakini baadaye akamwonea Mungu wivu, wivu wa madaraka, hivyo Mungu akamtupa duniani kwa sababu ya kupingana na utawala wake mtakatifu. Duniani Shetani akamtumia nyoka kama mdakale kumdanganya Hawa. Hawa na Adamu wakamsikiliza Shetani badala ya kumsikiliza Mungu, nao wakalaaniwa. Shetani akajidai kuwa alikuwa na uwezo wa kufanya uzao wote wa Adamu na Hawa uwe mbali na Mungu, hivyo Mungu akampa muda wa kujaribu na kuthibitisha madai yake, lakini Shetani mpaka leo bado hajafanikiwa. Wakiitawala dunia leo kwa udanganyifu wa hali ya juu, pamoja naye, ni baadhi ya malaika ambao Shetani alifanikiwa kuwalaghai huko mbinguni. Mungu akawalaani pia na kuwatupa huku duniani, ambako Shetani alipapenda zaidi.”
―
―

“Mungu alimuumba mwanadamu ili aitawale dunia. Shetani tayari alikuwepo wakati Adamu anaumbwa. Adamu na Hawa walipokula tunda la mti wa katikati, walikufa kiroho â€� Yaani, walipoteza sura na asili ya Mungu â€� Shetani akawashinda kuanzia kipindi hicho na kuendelea. Tulizaliwa katika dhambi. Kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Njia pekee ya kuikomboa sura na asili ya Mungu ni kumpokea Yesu (Kristo) kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.”
―
―

“Kuwepo kwa Mti wa Uzima wa Milele katika Bustani ya Edeni (pamoja) na Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya inamaanisha, Adamu na Hawa walikuwa hai kiroho mpaka walipokula tunda la mti wa katikati ambapo hali yao ya maisha ilibadilika. Adamu na Hawa walikufa lakini hawakufa â€� walikufa baadaye kabisa. Hii inamaanisha kwamba (haya ni mawazo yangu tu) mtu anapokufa anakuwa amekula tunda la mti wa katikati, litakalomwezesha kuendelea kuishi katika hali nyingine ya maisha ambayo sisi hatuijui.”
―
―

“Nini kingetokea kama Adamu na Hawa wasingekula tunda la Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya mpaka siku ya Sabato? Mungu angewaruhusu kula na lengo la uumbaji wa Mungu lingekamilika. Wanadamu wakifuata Amri Kumi za Mungu katika maisha yao watakuwa na uwezo maalumu ambao baadaye utawawezesha, kupitia Roho Mtakatifu, kuwa na maarifa ya siri ya uumbaji wa Mungu.”
―
―

“Dhambi ya Adamu ilileta mauti duniani (kwa viumbe vyote, si tu kwa binadamu). Hiyo ni kwa mujibu wa Biblia. Kisayansi si kweli; kwa sababu mauti yalikuwepo kabla Adamu na Hawa hawajaumbwa! Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Dhambi iliathiri uumbaji wote ikiwemo mimea, wanyama, wadudu na kila kitu kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu; ambavyo huteseka kwa sababu ya laana ya dunia. Kama wanyama na mimea visingekuwa vinakufa, binadamu wasingepata mahali pa kuishi. Hata hivyo, kifo cha Yesu msalabani kitafufua kila kitu â€� kitafufua uumbaji wote.”
―
―

“Kama miaka 1000 ya duniani ni sawa na siku moja ya Mungu; hivyo basi, miaka 930 aliyoishi Adamu ni sawa na siku 0.93 au saa 22:32 za Mungu. Kwa hiyo, ili siku ya Mungu itimie Adamu alipaswa kuishi miaka 70 (siku 0.07 au saa 1:68) zaidi! Ukiidadavua saa 1:68 unapata saa 2:08. Kulingana na muda wa mbinguni tunapaswa kuishi kwa muda wa saa 2:08! Muda huo ni mfupi sana.”
―
―

“Kulingana na muda wa Mungu, maisha ya Adamu yalikuwa siku 0.93 au saa 22:32! Maisha ya mwanadamu ni siku 0.07 au saa 1:68!”
―
―
All Quotes
|
My Quotes
|
Add A Quote
Browse By Tag
- Love Quotes 99.5k
- Life Quotes 78k
- Inspirational Quotes 74.5k
- Humor Quotes 44.5k
- Philosophy Quotes 30.5k
- Inspirational Quotes Quotes 27.5k
- God Quotes 26.5k
- Truth Quotes 24k
- Wisdom Quotes 24k
- Romance Quotes 23.5k
- Poetry Quotes 22.5k
- Life Lessons Quotes 20.5k
- Death Quotes 20.5k
- Happiness Quotes 19k
- Quotes Quotes 18.5k
- Hope Quotes 18k
- Faith Quotes 18k
- Inspiration Quotes 17k
- Spirituality Quotes 15.5k
- Religion Quotes 15k
- Motivational Quotes 15k
- Writing Quotes 15k
- Relationships Quotes 15k
- Life Quotes Quotes 14.5k
- Love Quotes Quotes 14.5k
- Success Quotes 13.5k
- Time Quotes 12.5k
- Motivation Quotes 12.5k
- Science Quotes 12k
- Motivational Quotes Quotes 11.5k