Å·±¦ÓéÀÖ

Siasa Quotes

Quotes tagged as "siasa" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Mungu alilibariki taifa la Israeli katika misingi ya kidini na si katika misingi ya kisiasa au misingi ya kihistoria; na asili ya dini ya Kikristo ni kutoka katika taifa hilo ambalo Biblia imelitaja kama taifa teule la Mwenyezi Mungu. Mgogoro wa Israeli na Palestina ulianzishwa na Israeli mwenyewe. Yakobo alipokea baraka iliyokuwa si ya kwake kwa kutumia hila ya Rebeka. Baraka ya Yakobo ilikuwa ya Esau.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usimwabudu mungu mwingine isipokuwa Mungu. Usimwabudu mtu, mnyama, sanamu, samaki, au usiziabudu fikira zako kichwani. Usiitumikie kazi, mali, mila, anasa, siasa, wala usiyatumikie mamlaka au usiutumikie umaarufu au ufahari, kuliko Mungu. Ukiithamini kazi, mali, mila, anasa, siasa au ukiyathamini mamlaka, au ukiuthamini umaarufu au ufahari zaidi kuliko Mungu, au ukiyapa majukumu yako muda mwingi zaidi kuliko Mungu umeabudu miungu; wakati ulipaswa kumwabudu Mungu peke yake. Usiwe na vipaumbele vingine vyovyote vile katika maisha yako zaidi ya Mungu, kwani Mungu ni Mungu mwenye wivu.”
Enock Maregesi

“Mimi ni mmoja kati ya wale wasiopenda maendeleo ya watu wachache au peke yako ndomana nimechagua mabadiliko katika maisha yangu sisubirii wanasiasa”
Chrisper Malamsha

“Tukiacha Siasa Zinazotutawala Ziingilie Dirishani, Hekima Zinazotutawala Pia Zitatutokea Mlangoni”
Wilson M Mukama