欧宝娱乐

Ufaransa Quotes

Quotes tagged as "ufaransa" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Radia Hosni, mhitimu wa mikanda miwili myeusi ya sanaa za mapigano za kareti na kung鈥檉u katika ngazi ya dani mbili za kung鈥檉u na dani moja ya kareti, mwanajeshi wa Tunisia aliyepata mafunzo ya kawaida ya kijeshi nchini Ufaransa na mafunzo ya kikomandoo nchini Uingereza kabla ya kujiunga na Tume ya Dunia, alikuwa mshindi wa tuzo ya shujaa wa taifa la Tunisia. Hussein Kashoggi alipokuwa akiwasili Tunis kutokea Copenhagen, Radia alikuwa katika Uwanja wa Mpira wa El Menzah akiangalia mechi kati ya Stade Tunisien na Esp茅rance ST 鈥� timu ambayo mchumba wake Fathi Meoki alikuwa kocha msaidizi. Fujo zilipozuka, baada ya Stade Tunisien kufungwa bao moja kwa sifuri na Esp茅rance ST, Radia alipanda Quadrifoglio na kuondoka kuelekea Uwanja wa Ndege wa Tunis-Carthage; ambapo alimpokea Hussein Kashoggi na jambazi wa Kolonia Santita, Delfina Moore.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ndege ya Kolonia Santita, Grumman Gulfstream III, tofauti na ndege alizokuwa akitumia Panthera Tigrisi na makompade wake wa karibu, ilifanya kazi kubwa katika mgogoro wa Kolonia Santita na Tume ya Dunia. Dar es Salaam Grumman ilipomchukua kachero Giovanna Garcia wa Kolonia Santita, baada ya ndege hiyo kutumwa na makamanda wa Kolonia Santita wa Copenhagen, ilimpeleka Paris nchini Ufaransa kuhudhuria kikao cha siri cha CS-Paris. Katika kikao hicho yeye na wenzake wakapanga mauaji ya Kamanda John Murphy Ambilikile, kwa kusuka mbinu kamambe za kumteketeza, kabla ndege yake haijafika Copenhagen. Giovanna akashiriki pia kupeleka taarifa za Murphy duniani kote katika matawi yote ya Kolonia Santita, Urusi ikiwemo, ambapo Murphy alitekwa nyara na CS-Moscow. Baada ya 'mauaji' ya Murphy, Grumman iliwapeleka baadhi ya maadui waliohusika na mauaji hayo Mexico City katika makao makuu ya Kolonia Santita; kisha ikarudi Copenhagen kumchukua kiongozi wa CS-Copenhagen, Regner Steiner Valkendorff, na Kachero wa Kolonia Santita Delfina Moore.”
Enock Maregesi