Å·±¦ÓéÀÖ

Uingereza Quotes

Quotes tagged as "uingereza" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Mahatma Gandhi alipigwa risasi na kufariki dunia baada ya maisha yake kumfelisha. Lakini kifo chake kiliipatia India uhuru kutoka Uingereza. Hivyo, akafanikiwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Radia Hosni, mhitimu wa mikanda miwili myeusi ya sanaa za mapigano za kareti na kung’fu katika ngazi ya dani mbili za kung’fu na dani moja ya kareti, mwanajeshi wa Tunisia aliyepata mafunzo ya kawaida ya kijeshi nchini Ufaransa na mafunzo ya kikomandoo nchini Uingereza kabla ya kujiunga na Tume ya Dunia, alikuwa mshindi wa tuzo ya shujaa wa taifa la Tunisia. Hussein Kashoggi alipokuwa akiwasili Tunis kutokea Copenhagen, Radia alikuwa katika Uwanja wa Mpira wa El Menzah akiangalia mechi kati ya Stade Tunisien na Espérance ST â€� timu ambayo mchumba wake Fathi Meoki alikuwa kocha msaidizi. Fujo zilipozuka, baada ya Stade Tunisien kufungwa bao moja kwa sifuri na Espérance ST, Radia alipanda Quadrifoglio na kuondoka kuelekea Uwanja wa Ndege wa Tunis-Carthage; ambapo alimpokea Hussein Kashoggi na jambazi wa Kolonia Santita, Delfina Moore.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wakati Yuda ikiongozwa na kiongozi mzuri na mwenye haki kama Yosia, taifa lilistawi. Lakini ilipokuwa chini ya mwovu Manase, taifa lilisambaratika. Katika karne hii, Uingereza ilipata msukosuko mkubwa mwaka 1936 juu ya uamuzi wa Edward VIII kuoa mwanamke wa Kimarekani aliyekuwa mtalaka Wallis Simpson. Uamuzi huo ulisababisha matatizo makubwa ya kikatiba, na nusura serikali ya Uingereza ijiuzuru. Hata hivyo, kaka yake mdogo, George VI, kwa mapenzi makubwa na nchi yake, huku akikataa katakata kuondoka London wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, aliliongoza taifa hilo katika kipindi kigumu zaidi kuliko vyote katika historia ya Uingereza. Kanuni hii ya uongozi ina ukweli katika jambo lolote kubwa na hata dogo la ujasiri.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiingereza kililetwa na wakoloni wa Kiingereza kutoka Uingereza na walikitumia katika masuala yote ya kiutawala ya Afrika Mashariki. Kililetwa pia na wamisionari waliojenga shule na kuwafundisha Kiingereza wanafunzi na walimu na watu wengine wa kawaida, kwa lengo la kuwasaidia katika kazi yao ya kueneza dini kama wakalimani, hivyo kufanya Kiingereza kienee zaidi kuliko Kiswahili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna tetesi kuwa Julius Nyerere alipewa tuzo ya MBE na malkia wa Uingereza akiwa rais wa Tanzania! Lakini aliikataa! Kwa nini? Kwa sababu angeonekana Mwingereza zaidi kuliko Mtanzania! Januari 26, 1996 akapewa Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Mahatma Gandhi ya mwaka 1995, ya kwanza kabisa, iliyotolewa na Serikali ya India. Lakini hiyo pia akaikataa! Kwa sababu Mahatma Gandhi alimwaga damu katika harakati zake za kuwang'oa wakoloni barani Afrika! Kama ni kweli, hakuna kujitolea kuliko huko.”
Enock Maregesi