Ujumbe Quotes
Quotes tagged as "ujumbe"
Showing 1-3 of 3

“Kujua nini kitatokea kesho, au kesho kutwa, au kujua jinsi usaili wako wa kazi utakavyokuwa, au ni maswali gani utakayoulizwa kwenye mtihani kwa mfano, kutarahisisha sana maisha yetu. 'Madirisha' madogo katika kipindi cha saa za usoni hufunguka mara kwa mara katika maisha yetu, kimiujiza na bila kutegemea. Hudokeza kidogo jinsi tukio fulani, au hali fulani, au kitu fulani kitakavyotokea katika kipindi cha wakati ujao bila sisi wenyewe kujua. Hali hii hujulikana kama jakamoyo. Jakamoyo ni sanaa ya kubashiri vitu visivyojulikana. Kazi yake ni kutuhadharisha na kutusaidia! Kujua mapema hatari iliyoko mbele yako inamaanisha kuwa na uwezo wa kujilinda kutokana na hatari hiyo, na kuwa na uwezo wa kuepuka mitego. Jakamoyo huweza kumtokea mtu katika hali ya 'maono', au 'mwako wa mwanga' (yaani kufumba na kufumbua). Mara nyingi huonekana kama ndoto. Hutokea wakati mtu amelala usingizi. Ikitokea wakati mtu yuko macho, wakati mwingine huendana na misisimko ya mwili kabla ya mwako, ikiwa na maana ya kumfanya mtu awe makini na kitu chochote kinachotarajia kutokea. Ndiyo maana baadhi ya watu utakuta wakisema wanaumwa tumbo, kifua au kichwa cha ghafla katika kipindi ambacho taswira ya tukio fulani inakuwa ikitokea akilini mwao, ikiwaambia waende mahali fulani bila kukosa kwa mfano, na kadhalika. Hakuna mtu anaweza kufanya jakamoyo imtokee. Hutokea yenyewe muda wowote kuleta ujumbe, kuhusiana na matukio ya wakati ujao. Kamwe usipuuze wito wa moyo wako.”
―
―

“Unabii ni uwezo alionao mtu wa kuongea mambo matakatifu ya Mungu, kuwaongoza wenzake katika njia njema. Mungu humwambia nabii kitu cha kusema na nabii huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Mungu hawezi kuongea na watu mpaka watu wajue jinsi ya kuongea naye, na wakati mwingine ni rahisi sana kusikia ujumbe kutoka kwa mtu kuliko kuusikia ujumbe huo moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Mungu anaweza kukwambia useme kitu fulani kwa mtu au watu fulani. Unaweza usijue kwa nini anakwambia ufanye hivyo, lakini utajisikia msukumo wa hali ya juu wa kutangaza ujumbe uliopewa kuuwasilisha. Mungu hatakulazimisha, lakini atakung’ang’aniza, na ni Mungu pekee anayejua lengo la mawasiliano hayo. Mungu akikwambia ufanye kitu fanya mara moja, usiulize kwa nini. Kazi yako ni kufanya unachotakiwa kufanya, kusema unachotakiwa kusema, si kuuliza maswali. Mtumie rafiki yako wa kiroho kukuongoza katika mema na mabaya, na usitambe â€� kwamba unaongea maneno uliyoambiwa na Mungu uyaongee. Ukiwa na uwezo mkubwa wa kuongea na Mungu utaleta mabadiliko katika dunia.”
―
―

“Ukiwa makini, nadhani, utapata maana ya ujumbe unaopewa na Roho Mtakatifu kwa wale wanaomwamini Mungu au ‘daemonâ€� (tofauti na ‘demonâ€�) kwa wale wasiomwamini Mungu. Mimi, kwa mfano, huwa najali muda. Jicho langu likicheza au kiungo changu chochote cha mwili kikiuma ghafla na kuacha, au hata kisipoacha, jambo lolote ninalolifikiria muda huo ambapo jicho linacheza au kiungo changu cha mwili kinauma najua ni ujumbe kutoka kwa Mungu na una uhusiano na jambo hilo ninaloliwaza. Hivyo, kuanzia sekunde hiyo napaswa kuwa makini sana na jambo lolote ninalolifikiria.”
―
―
All Quotes
|
My Quotes
|
Add A Quote
Browse By Tag
- Love Quotes 99.5k
- Life Quotes 78k
- Inspirational Quotes 74.5k
- Humor Quotes 44.5k
- Philosophy Quotes 30.5k
- Inspirational Quotes Quotes 27.5k
- God Quotes 26.5k
- Truth Quotes 24k
- Wisdom Quotes 24k
- Romance Quotes 23.5k
- Poetry Quotes 22.5k
- Life Lessons Quotes 20.5k
- Death Quotes 20.5k
- Happiness Quotes 19k
- Quotes Quotes 18.5k
- Hope Quotes 18k
- Faith Quotes 18k
- Inspiration Quotes 17k
- Spirituality Quotes 15.5k
- Religion Quotes 15k
- Motivational Quotes 15k
- Writing Quotes 15k
- Relationships Quotes 15k
- Life Quotes Quotes 14.5k
- Love Quotes Quotes 14.5k
- Success Quotes 13.5k
- Time Quotes 12.5k
- Motivation Quotes 12.5k
- Science Quotes 12k
- Motivational Quotes Quotes 11.5k