Å·±¦ÓéÀÖ

Ulinzi Quotes

Quotes tagged as "ulinzi" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Mlinzi mmoja wa ndani alishtuka aliposikia kishindo cha kitu kudondoka. Aligeuka upesiupesi lakini akaridhika alipokuta ni mwenzake ila akashindwa kuelewa kwa nini mwenzake huyo aanguke. Hata hivyo aliachana na Murphy na kuendelea na lindo lake huku akivuta msokoto mfupi wa bangi. Lakini, yule mlinzi hakutembea hatua nyingi kabla ya kusimama na kujiuliza maswali kichwani. Kwa nini mwenzake huyo atoke nje ambako ndiko alikuwa amepangiwa na ambako ndiko waliambiwa kuwe na ulinzi imara na ndiyo maana wakawekwa saba? Kwa nini aanguke ndani ya ua bila hata ya kumsemesha chochote? Kwa nini hakumpigia redio kwamba alikuwa akiingia ndani ili asiwe na wasiwasi? Alipowaza sana aliamua asiwe na pupa. Aliamua kumfuata mwenzake, aliyekuwa mbele yake, ili amwambie kitu na washirikiane.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Watoto hawatakiwi kuchungwa kupita kiasi hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho. Uhuru utakaowanyima wakiwa wadogo watakuja kuutafuta baadaye wakiwa wakubwa. Wakiutafuta baadaye wakiwa wakubwa hawataeleweka vizuri katika jamii. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata lakini si uhuru wa kila kitu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Vijana wa Tume walipofika kambini chini ya ulinzi mkali wakiwa na Kahima, polisi wengi walionekana kuwapigia saluti lakini wakubwa wao wakawakataza na kuwambia wao walikuwa watu wa kawaida kama wao. Walisindikizwa na lundo la polisi mpaka ndani ya jumba la utawala Murphy alimokuwa ameuhifadhi mwili wa Radia. Walipofika walishtuka, na hata kuwashangaza polisi. Mwili wa Radia haukuwepo! Walitafuta kila sehemu, na kuwambia polisi wawasaidie kutafuta, lakini Radia alishapotea. Murphy alipata wazo na kutoka nje, kwa kukimbia, polisi wengi wakimfuata; mpaka katika helikopta ya DEA ambapo alifungua mlango na kuingia ndani. Ndani ya helikopta hakukuwa na mtu!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Mungu ana uwezo wa kukuwekea ulinzi kulia na kushoto yaani anayekulinda naye ana mlinzi wake. Lakini wakati mwingine anaacha ufuate kile ambacho moyo wako unataka kwa sababu hataki kukulazimisha ijapokuwa uwezo huo anao. Mungu hakukuumba kuwa roboti. Alikuumba kuwa huru kuchagua mema au mabaya usije ukamlaumu baadaye kwamba ulimchagua yeye kwa sababu hukuwa na uhuru. Msikilize Roho wa Mungu, kabla na katika kila jambo unalofanya.”
Enock Maregesi