Redio Quotes
Quotes tagged as "redio"
Showing 1-4 of 4

“John Murphy amefariki dunia. Ndege aliyotoka nayo hapa, Dar es Salaam, ndiyo aliyotoka nayo Paris na ndiyo hiyo iliyoanguka katika mazingira ya kutatanisha. Watu waliobahatika kuing鈥檃mua fununu hii ni wachache na ambao hivi sasa hawajiwezi kabisa, akiwemo kamishna wetu wa kanda Profesa Mafuru. Profesa yuko mahututi. Ameshtuka baada ya kusikia taarifa hizo katika redio ya hapa. Yuko chini ya uangalizi mkali wa madaktari. Mungu aiweke roho ya John Murphy, shujaa wa karne, mahali pema peponi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Mlinzi mmoja wa ndani alishtuka aliposikia kishindo cha kitu kudondoka. Aligeuka upesiupesi lakini akaridhika alipokuta ni mwenzake ila akashindwa kuelewa kwa nini mwenzake huyo aanguke. Hata hivyo aliachana na Murphy na kuendelea na lindo lake huku akivuta msokoto mfupi wa bangi. Lakini, yule mlinzi hakutembea hatua nyingi kabla ya kusimama na kujiuliza maswali kichwani. Kwa nini mwenzake huyo atoke nje ambako ndiko alikuwa amepangiwa na ambako ndiko waliambiwa kuwe na ulinzi imara na ndiyo maana wakawekwa saba? Kwa nini aanguke ndani ya ua bila hata ya kumsemesha chochote? Kwa nini hakumpigia redio kwamba alikuwa akiingia ndani ili asiwe na wasiwasi? Alipowaza sana aliamua asiwe na pupa. Aliamua kumfuata mwenzake, aliyekuwa mbele yake, ili amwambie kitu na washirikiane.”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Wakiwa na suti nzito za kijani na madoa meusi (鈥楪hillie Suits鈥�) kwa ajili ya kupigania porini; Vijana wa Tume walikuwa na kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (iliyokuwa na uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migongoni mwao juu ya vizibao vya kuzuia risasi, vitibegi vya msalaba mwekundu (鈥楤lowout Kits鈥� 鈥� katika mapaja ya miguu yao ya kulia, ndani yake kukiwa na pisto na madawa ya huduma ya kwanza), vitibegi vya kujiokolea (鈥楨vasion Kits鈥� 鈥� katika mapaja ya miguu yao ya kushoto, ndani yake kukiwa na visu na pesa na ramani ya Meksiko) na bunduki za masafa marefu. Kadhalika, Vijana wa Tume waliamua kuchukua Punisher 鈥� waliyoafikiana baadaye kuwa ilikuwa nzuri kuliko RPG-7, 鈥楻ocket Propelling Gun鈥�, ambayo Mogens alipendekeza waitumie kubomolea Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals; kwa sababu hakutaka kuleta madhara kwa watu waliokuwa hawana hatia.”
― Kolonia Santita
― Kolonia Santita

“Kofia za chuma au sandarusi zenye uwezo wa kukwepesha risasi za wadunguzi na kuzuia mpaka risasi tatu za AK-47, ijapokuwa zimetengenezwa kuzuia risasi moja tu, ni miongoni mwa vitu 17 vilivyobebwa na makomandoo wa Tume ya Dunia; wakati wakitekeleza Operesheni ya Kifo au Ushindi Kamili (operesheni ndogo ya Operation Devil Cross ya Tume ya Dunia) katika Msitu wa Benson Bennett, Salina Cruz, Oaxaca, nchini Meksiko. Thamani ya vitu vya komandoo mmoja wa EAC ('Executive Action Corps') akiwa vitani ni zaidi ya dola za Kimarekani 65,000; ikiwa ni pamoja na magwanda ya jeshi ('Ghillie Suits'), kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (yenye uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migongoni mwao juu ya vizibao vya kuzuia risasi, vitibegi vya msalaba mwekundu ('Blowout kits' 鈥� katika mapaja ya miguu yao ya kulia, ndani yake kukiwa na pisto na madawa ya huduma ya kwanza), vitibegi vya kujiokolea ('Evasion Kits' 鈥� katika mapaja ya miguu yao ya kushoto, ndani yake kukiwa na visu na pesa na ramani ya Meksiko) na bunduki za masafa marefu.”
―
―
All Quotes
|
My Quotes
|
Add A Quote
Browse By Tag
- Love Quotes 99.5k
- Life Quotes 78k
- Inspirational Quotes 74.5k
- Humor Quotes 44.5k
- Philosophy Quotes 30.5k
- Inspirational Quotes Quotes 27.5k
- God Quotes 26.5k
- Truth Quotes 24.5k
- Wisdom Quotes 24k
- Romance Quotes 24k
- Poetry Quotes 23k
- Life Lessons Quotes 21k
- Death Quotes 20.5k
- Quotes Quotes 19k
- Happiness Quotes 19k
- Hope Quotes 18k
- Faith Quotes 18k
- Inspiration Quotes 17k
- Spirituality Quotes 15.5k
- Religion Quotes 15k
- Motivational Quotes 15k
- Writing Quotes 15k
- Relationships Quotes 15k
- Life Quotes Quotes 14.5k
- Love Quotes Quotes 14.5k
- Success Quotes 13.5k
- Time Quotes 12.5k
- Motivation Quotes 12.5k
- Science Quotes 12k
- Motivational Quotes Quotes 11.5k