欧宝娱乐

Zaka Quotes

Quotes tagged as "zaka" Showing 1-7 of 7
Enock Maregesi
“Zaka huondoa laana ya mapato.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Zaka husaidia kueneza injili duniani kote. Ukitoa zaka umesaidia kueneza injili duniani kote. Toa zaka na mapato yako yatabarikiwa. Usitoe zaka na mapato yako yatalaaniwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani akikupa hela chukua. Hiyo hela ameiiba kutoka kwa Baba. Ukishaichukua, toa zaka.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Katika dunia ya leo ambapo mamilioni ya watu hutegemea utandawazi kupata pesa, kuwa na imani kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua au mtu mwenye nia mbaya na wewe ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa sababu, karibu kila mtu unayekutana naye ni Shetani. Shetani ni mtu yoyote mwenye nia mbaya na wewe. Hivyo, kama uliwahi kuambiwa kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ni kitu kibaya futa imani hiyo. Utaachaje kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua wakati kila siku unamwomba Mungu akusaidie, na Mungu hutenda kazi zake pale tunapojisahau? La sivyo hutapata pesa unayotamani kupata katika maisha yako, na kamwe hutawaamini watu. Zaka huondoa laana ya mapato. Toa zaka kununua pepo uliyopewa na Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu hataki tuwe maskini, kwani fedha na dhahabu ni mali yake. Anachotaka kutoka kwetu, zaka.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa itolewe kwa masharti au bila masharti chukua, kwani huyo aliyeitoa si yake. Benki, kwa mfano, ikitaka kukupa mkopo itakuwa na masharti yake; chukua, iwapo utakubaliana na masharti hayo. Jambazi akikupa pesa ili ukafanyie ujambazi chukua pia. Lakini hiyo usiipeleke kanisani, ipeleke serikalini. Serikali itajua jinsi ya kupambana na huyo aliyekupa hiyo pesa, na hiyo pesa itaendelea kuimarisha ulinzi na usalama nchini. Pesa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama nchini ni sawa na zaka, au sadaka, na wewe utabarikiwa kwa kupata nyingine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hata kama umetajirika kiasi gani mpe Mungu kipaumbele cha kwanza katika kila jambo unalofanya. Toa zaka na sadaka na jitolee katika mambo yote yanayompendeza Mungu.”
Enock Maregesi