欧宝娱乐

Mwanao Quotes

Quotes tagged as "mwanao" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Kila binadamu hapa duniani ni wa thamani kubwa. Chochote utakachofanya, kizuri au kibaya, kidogo au kikubwa, kitabadilisha maisha ya watu. Ukiwa na msingi mzuri kwa mwanao ataishi vizuri atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mkubwa wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Ukiwa na msingi mbaya kwa mwanao ataishi vibaya atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mdogo wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Kuwa mkarimu kwa mazingira, kuwa mkarimu kwa wanyama, kuwa mkarimu kwa binadamu wenzako, kwa faida ya vizazi vijavyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama ulikuwa ukimwambia mwanao kuwa atakuwa jambazi labda kwa sababu ya fujo zake alipokuwa mdogo, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota atakapopevuka akili ni ya kihalifu. Kwani hayo ndiyo mambo ya kwanza kabisa kujirekodi katika ubongo wake alipokuwa hajitambui. Lakini kama ulikuwa ukimwambia kuwa atakuwa daktari au mwanasheria, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota ni ya kidaktari au kisheria. Kuna uwezekano mkubwa akawa daktari au mwanasheria baadaye katika maisha yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tengeneza maisha ya mwanao kwa kuongea naye maneno mazuri anapokuwa tumboni mwako, na anapokuwa ananyonya akikuangalia machoni.”
Enock Maregesi