欧宝娱乐

Binadamu Quotes

Quotes tagged as "binadamu" Showing 1-26 of 26
Enock Maregesi
“Kila binadamu hapa duniani ni wa thamani kubwa. Chochote utakachofanya, kizuri au kibaya, kidogo au kikubwa, kitabadilisha maisha ya watu. Ukiwa na msingi mzuri kwa mwanao ataishi vizuri atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mkubwa wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Ukiwa na msingi mbaya kwa mwanao ataishi vibaya atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mdogo wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Kuwa mkarimu kwa mazingira, kuwa mkarimu kwa wanyama, kuwa mkarimu kwa binadamu wenzako, kwa faida ya vizazi vijavyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hakuna shaka yoyote (kwa mfano) kwamba mboga za majani na matunda vina vitamini nyingi mwilini na madini na vitu vyote vizuri katika mwili wa binadamu, na kwamba kadhalika vina kirutubisho cha ufumwele ambacho huzuia kufunga choo na matatizo mengine ya mfumo wa usagaji chakula. Kirutubisho hiki kikizidi mwilini utapata matatizo makubwa yatakayoweza hata kukusababishia kifo!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥�, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi.

Wanaendelea kusema kuwa baada ya 鈥楤ig Bang鈥� kutakuwepo na 鈥楤ig Crunch鈥�, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena.

Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥� ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya 鈥楤ig Crunch鈥�, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia.

Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu 鈥� badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri 鈥� sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea.

Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa 鈥榙ark matter鈥�, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo 鈥榤ultiverse鈥� au 鈥榤eta-universe鈥�.

Kuna kitu kinaitwa 鈥楬iggs boson鈥� 鈥� chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (鈥榤ass鈥�) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 鈥楤ig Bang鈥� miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa 鈥榚poch鈥� 鈥� ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥�, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni.

Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya 鈥榙ark matter鈥�, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha 鈥楽tandard Model鈥� litapatikana.

Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana 鈥楬iggs boson鈥� mwaka 1993 iliitwa 鈥楾he God Particle鈥�. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata.

Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wana uwezo wa kupeleleza hadi kipindi cha karne ya kwanza ambapo Yesu aliishi, alikufa, alifufuka na alipaa kwenda mbinguni, na wana uwezo wa kujua mambo mengi kwa hakika yaliyofanyika katika kipindi hicho na hata katika kipindi cha kabla ya hapo.

Kuna miujiza ambayo Yesu aliifanya ambayo haiko ndani ya Biblia. Kwa mfano, Biblia inasema Yesu alizaliwa ndani ya zizi la ng鈥檕mbe wakati sayansi inasema alizaliwa nje ya zizi la ng鈥檕mbe; na muujiza wa kwanza kuufanya ambao hauko ndani ya Biblia ni kutembea mara tu baada ya kuzaliwa, na watu na ndege wa angani kuganda kabla ya kuzaliwa Masihi na kabla ya wakunga kufika kumsaidia Maria Magdalena kujifungua.

Akiwa na umri wa miaka sita, sayansi inasema, Yesu alikuwa akicheza na mtoto mwenzake juu ya paa la nyumba ya jirani na mara Yesu akamsukuma mwenzake kutoka juu hadi chini na mwenzake huyo akafariki papo hapo. Watu walipomsonga sana Yesu kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mwenzake, na kwamba wangemfungulia mashtaka, Yesu alikataa katakata kuhusika na kifo hicho.

Lakini walipozidi kumsonga, aliusogelea mwili wa rafiki yake kisha akamwita na kumwambia asimame. Yule mtoto alisimama! Huo ukawa muujiza mkubwa wa kwanza wa Yesu Kristo, kufufua mtu nje ya maandiko matakatifu.

Kuna mifano mingi inayodhihirisha uwepo wa Mungu ambayo wanasayansi hawawezi hata kuipatia majibu. Tukio la Yoshua kusimamisha jua limewashangaza wanasayansi hadi nyakati za leo. Mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walijaribu kurudisha muda nyuma kwa kompyuta kuona kama kweli wangekuta takribani siku moja imepotea kama ilivyorekodiwa katika Biblia.

Cha kushangaza, cha kushangaza mno, walikuta saa 23 na dakika 20 zimepotea katika mazingira ambayo hawakuweza na hawataweza kuyaelewa. Walipochunguza vizuri walikuta ni kipindi cha miaka ya 1500 KK (Jumanne tarehe 22 Julai) ambacho ndicho tukio la Yoshua la kusimamisha jua na kusogeza mwezi nyuma digrii 10, ambazo ni sawa na mzunguko wa dakika 40, lilipotokea.

Kwa kutumia elimu ya wendo, elimu ya kupanga miaka na matukio ya Kibiblia, dunia iliumbwa Jumapili tarehe 22 Septemba mwaka 4000 KK. Hata hivyo, mahesabu ya kalenda yanaonyesha kuwa Septemba 22 ilikuwa Jumatatu (si Jumapili) na kwamba kosa hilo labda lilisababishwa na siku ya Yoshua iliyopotea.

Hayo yote ni kwa mujibu wa Profesa C. A. Totten, wa Chuo Kikuu cha Yale, katika kitabu chake cha 鈥楯oshua鈥檚 Long Day and the Dial of Ahaz: A Scientific Vindication and a Midnight Cry鈥� kilichochapishwa mwaka 1890.

Kama hakuna Mungu iliwezekanaje Yoshua aombe jua lisimame na jua likasimama kweli? Iliwezekanaje Yesu aseme atakufa, atafufuka na atapaa kwenda mbinguni na kweli ikatokea kama alivyosema? Ndani ya Biblia kuna tabiri 333 zilizotabiri maisha yote ya Yesu Kristo hapa duniani na zote zilitimia 鈥� bila kupungua hata moja. Utasemaje hapo hakuna Mungu? Mungu yupo, naamini, sijui.

Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni si la vitabu vitakatifu pekee, hata sayansi inakubaliana na hilo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wa zamani katika Agano la Kale walikuwa wakiabudu miungu iliyotengenezwa kwa mawe na vinyago. Miungu hiyo haikuwa na chochote ndani mbali na kutengenezwa kwa akili na fikira za kibinadamu. Hii ilikuwa ni kinyume cha ukweli wa Kibiblia kwamba Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake, lakini si mtu aliyejaa dhambi kumtengeneza Mungu kwa mfano wake. Kuabudu miungu mingine ni dhambi kubwa. Tii Amri Kumi za Mungu; hasa ya kwanza, ya pili na ya tatu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani angekuwa na uwezo wa kuona ndani ya moyo wa mtu, binadamu angeshatengeneza moyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani angekuwa na uwezo wa kuona ndani ya ufahamu wa mtu, binadamu angeshatengeneza ubongo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ndoto ni lugha ya roho inayozungumza kimafumbo kumfanya binadamu ajitambue.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dhambi ya Adamu ilileta mauti duniani (kwa viumbe vyote, si tu kwa binadamu). Hiyo ni kwa mujibu wa Biblia. Kisayansi si kweli; kwa sababu mauti yalikuwepo kabla Adamu na Hawa hawajaumbwa! Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Dhambi iliathiri uumbaji wote ikiwemo mimea, wanyama, wadudu na kila kitu kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu; ambavyo huteseka kwa sababu ya laana ya dunia. Kama wanyama na mimea visingekuwa vinakufa, binadamu wasingepata mahali pa kuishi. Hata hivyo, kifo cha Yesu msalabani kitafufua kila kitu 鈥� kitafufua uumbaji wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ser bom para o ambiente. Seja gentil com os animais. Seja gentil com as pessoas. Se voc锚 fizer isso, voc锚 vai deixar uma marca no mundo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani alikuwa kiumbe mzuri kuliko wote mbinguni na ulimwenguni. Mungu alimpendelea. Alikuwa mzuri kuliko malaika wote na alikuwa na nguvu kuliko kiumbe mwingine yoyote yule aliyeumbwa na Mungu, akiwemo binadamu. Lakini alipotupwa kutoka mbinguni kuja duniani kama Adamu na Hawa walivyotupwa kutoka bustanini kuja duniani, Shetani alipoteza sifa yake. Alipoteza sifa yake kwa sababu ya dhambi aliyoitenda, dhambi ya kiburi, na kwa sababu ya kuwa mbali na utukufu wa mbinguni. Badala ya kuwa kiumbe mzuri kuliko wote, Shetani akawa kiumbe mbaya kuliko wote. Mungu akaahidi kutokumsamehe, kwa sababu yeye ndiye kiumbe wa kwanza kutenda dhambi mbinguni na ulimwenguni, kwani hakushawishiwa na mtu kumuasi Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Roho haina mifumo ya ufahamu! Haina pua, haina macho, haina ladha, haina harufu wala haina masikio. Kwa sababu roho haina mifumo ya ufahamu mtu, anapokufa mifumo yake yote 21 aliyokuwa nayo binadamu huoza na kuwa udongo. Hivyo, kuongea na mtu aliyekufa ni sawa na kuongea na udongo ukitegemea udongo huo ukusikie au uongee na wewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, bali alichaguliwa kuleta mabadiliko katika dunia kama Rais wa Tume ya Dunia kutetea afya na amani ya dunia nzima kwa unyenyekevu na heshima kwa binadamu wenzake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu ya Mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi. Mungu hauwi, Anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Ukifunikwa na damu ya Mwanakondoo Shetani, ambaye ni wakala, hatakuona. Lakini Mungu atakuona. Bila kafara ya damu hakuna msamaha wa dhambi. Bila kafara ya damu hakuna mafanikio.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna nguzo saba ambazo hazina budi kuzingatiwa kama unataka kuheshimiwa na kuwaheshimu wengine. Kwanza kabisa jitambue: wewe ni nani na unafanya nini hapa duniani. Halafu, kabla ya kusema jambo lolote kwa mtu yoyote fikiria kwanza maana au madhara ya hilo unalotaka kulisema. Kisha jifunze tamaduni mbalimbali na watendee wengine kama vile unavyotaka kutendewa au kama vile wanavyotaka kutendewa. Jifunze kusamehe na kusuluhisha migogoro katika jamii unamoishi huku ukidumisha heshima na utu kwa binadamu wenzako. Jijengee imani kwa watu, punguza upendeleo, fanya kazi kama timu kwani hakuna 鈥榤imi鈥� katika umoja ila kuna 鈥榮isi鈥�, na jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE kwa manufaa ya wote. Kuwa kiongozi katika kila jambo unalofanya na katika kila kitu unachofanya. Jitahidi kufanya jambo au kitu kwa usahihi kwa kadiri utakavyoweza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani anapenda damu kumtumia Mungu kwa faida yake kama vile Mungu anavyomtumia Shetani kwa faida yake. Mungu anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu, na Shetani anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Mungu anaishi ndani ya damu na damu ina nguvu kuliko Shetani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y. Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo, katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya Adamu, ambayo bado haijatakaswa. Damu ya Yesu si kitu kidogo. Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa. Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ni mtakatifu na kwa maana hiyo hatendi dhambi. Hivyo, hauwi wala hatesi. Tunajiua na kujitesa wenyewe. Ametupa hiari ya kuchagua mema au mabaya. Lakini anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu pale tunapoenenda sawasawa na machukizo yake. Damu ina nguvu kuliko Shetani na ina nguvu kuliko kuzimu. Unapojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani hataweza kukuona. Hivyo, hataweza kukudhuru. Lakini usipojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani atakuona. Hivyo, atakudhuru. Atakudhuru kwa sababu Mungu atakuwa ameruhusu akudhuru, kwa sababu ya uhuru wa kuchagua mema au mabaya aliotupatia, ijapokuwa ana uwezo wa kuzuia asikudhuru. Kwa mtindo huo Mungu anakuwa ametoa adhabu kwa binadamu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani naye anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu kwa sababu Shetani siku hizi anaishi makanisani na misikitini. Anamtumia Mungu kwa maana ya kutuingiza dhambini huku tunaona, tukiwa mbele ya uwepo wa Mungu tunayemwabudu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuwa mkarimu kwa mazingira, kuwa mkarimu kwa wanyama, kuwa mkarimu kwa binadamu wenzako, kwa faida ya vizazi vijavyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ni baba yetu wa kiroho. Hivyo basi, tunajua ya kuwa upendo wake umehifadhiwa ndani ya mioyo yetu. Kwa hiyo, kila mtu ana upendo wa 鈥榓gape鈥� kwa kiasi fulani; lakini si upendo kamili. Upendo wa 鈥榓gape鈥� kati ya binadamu na binadamu unahusiana na upendo wa kujitolea kwa ajili ya binadamu wengine. Kila mtu ana kiasi fulani cha upendo huo. Mtu akitaka awe na upendo kamili wa 鈥榓gape鈥� sharti awe mtiifu na mnyenyekevu mbele za Mungu, na mbele ya binadamu wenzake, sharti ampende Mungu, na sharti ampende jirani yake kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Injili tunayohubiriwa haina ugumu wowote. Mungu anatutaka tuamini na tunapoamini, tunapopata ufahamu na kuamini kuwa Mwana wa Mungu alikuwa binadamu kama sisi ili sisi tupate kuokolewa, upofu wetu wa kiroho unaanza kuondolewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Binadamu ni barua!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu alikuwa binadamu ili afe kama binadamu kwa ajili ya binadamu. Alikufa msalabani ili sisi wote tuokoke. Lakini Shetani hataki hilo litokee. Akiingilia uumbaji wa Mungu toka tumboni mwa binadamu, binadamu atakayezaliwa hatakuwa na uwezo wa kuongoka. Atakuwa na roho ya jini itakayomjua Shetani badala ya kumjua Mungu. Hivyo kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili hakutakuwa na maana, kwa sababu hakutakuwepo na mtu wa kuokolewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Haiwezekani binadamu kuridhika.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watoto wadogo wanakufa. Watu wazima wasiokuwa na hatia wanakufa vitani na katika majanga mengine ya asili. Kwa nini? Watoto wadogo wanaokufa walikuja duniani kufanya nini? Kwa nini watu wasiokuwa na hatia wanakufa ilhali Mungu yupo na asiwaepushe na matatizo ya dunia hii? Kama aliweza kuzuia binadamu wasiishi majini kwa sababu watakufa kwa nini asizuie matatizo yasiwapate watoto na watu wazima wasiokuwa na hatia? Sisi ni wadogo sana na Mungu ni mkubwa mno. Jibu hatutaweza kulielewa pamoja na kwamba tumepewa. Hata hivyo, Mungu hababaishwi na mwili. Anababaishwa na roho.”
Enock Maregesi