Å·±¦ÓéÀÖ

Neno La Mungu Quotes

Quotes tagged as "neno-la-mungu" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Usipoangalia kwa undani sana, mapepo wanatutawala kwa sababu hatuna uwezo wa kuwaona. Aidha, wanaweza, bila hata sisi kujua, kuwasiliana nasi kimawazo na kitabia kupitia hewa hiihii inayotusaidia katika kuishi. Watu wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani na mapepo wake hawataki tujue kama wanatudanganya au wameshatudanganya tayari, na hawataki tujue kama wako hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini. Licha ya hili jambo kutokea katika maisha yetu, Shetani bado anaweza kutudanganya hadi pale tutakapoerevuka kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha kwamba udanganyifu huo hautatokea tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hata hivyo, Shetani anaweza kutudanganya kupitia tamaduni zetu tulizozaliwa nazo. Utamaduni, dunia tunapoishi, ndiyo chanzo cha udanganyifu huu. Yesu Kristo alikufa msalabani ili tupate uhuru kutoka kwa Shetani. Chukua hatua sasa kwa sababu Shetani anaweza kukuteka, na kukufanya mtumwa tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Neno la Mungu tunalojifunza sasa litatufanya tuusimamie ukweli, uliodhihirishwa na mitume, katika kipindi cha dhiki kuu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mtu akikupiga ngumi utaumia. Akikutukana utaumia. Akikunyima Neno la Mungu utaumia pia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wenye mamlaka wana dhamana za mamlaka zao kama watumishi wa Mungu, kwa sababu Neno la Mungu liko wazi kwamba Mungu ndiye aliyewapa mamlaka hayo.”
Enock Maregesi