Å·±¦ÓéÀÖ

Madhara Quotes

Quotes tagged as "madhara" Showing 1-6 of 6
Enock Maregesi
“Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya 'hydrogen cyanide'. Gesi ya 'hydrogen cyanide' ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha 'cyanide' atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi â€� kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote â€� hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wakiwa na suti nzito za kijani na madoa meusi (‘Ghillie Suitsâ€�) kwa ajili ya kupigania porini; Vijana wa Tume walikuwa na kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (iliyokuwa na uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migongoni mwao juu ya vizibao vya kuzuia risasi, vitibegi vya msalaba mwekundu (‘Blowout Kitsâ€� â€� katika mapaja ya miguu yao ya kulia, ndani yake kukiwa na pisto na madawa ya huduma ya kwanza), vitibegi vya kujiokolea (‘Evasion Kitsâ€� â€� katika mapaja ya miguu yao ya kushoto, ndani yake kukiwa na visu na pesa na ramani ya Meksiko) na bunduki za masafa marefu. Kadhalika, Vijana wa Tume waliamua kuchukua Punisher â€� waliyoafikiana baadaye kuwa ilikuwa nzuri kuliko RPG-7, ‘Rocket Propelling Gunâ€�, ambayo Mogens alipendekeza waitumie kubomolea Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals; kwa sababu hakutaka kuleta madhara kwa watu waliokuwa hawana hatia.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kula sana kunaweza kusababisha virutubisho kuzidi mwilini zaidi ya kiwango kinachohitajika na mwili, ambavyo baadaye vinaweza kusababisha madhara ya papo kwa hapo kama tumbo kuuma au tumbo kujaa gesi! Baada ya muda mrefu wingi wa virutubisho hivi unaweza kuingiliana na ufyonzaji wa madini kama fosforasi, kalisi, magnesi, chuma, na zinki, hali inayoweza kusababisha upungufu mkubwa wa virutubisho, unaoweza kusababisha kifo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kujua ukweli juu ya uraibu wa madawa ya kulevya kunaweza kumsaidia mtu kujua madhara ya madawa ya kulevya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ili kupambana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika jamii ya Tanzania, ni muhimu kutoa elimu kwa Watanzania juu ya madhara yanayoambatana na matumizi ya madawa hayo. Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya kulevya pia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kasoro za Uzi zilizofanya zisitumiwe tena na kikosi cha usalama cha rais wa Marekani ni kutokuwa na shabaha imara katika umbali mfupi (hutawanya risasi na huleta madhara makubwa katika umbali mfupi hivyo kuweza kudhuru hata watu wasiokuwa na hatia) na kutokuwa na uwezo wa kutoboa kinga ya risasi dhidi ya magaidi wanaotumia mavazi ya kuzuia risasi, wanaotishia usalama wa rais wa Marekani. Gaidi mwenye mavazi ya kuzuia risasi aliweza kumdhuru rais kwa maana ya USSS kushindwa kumdhibiti. Badala yake, sasa USSS wanatumia FNP90 â€� zenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi, na ambazo hazileti madhara makubwa katika umbali mfupi na katika umbali mrefu. Bunduki hizi, zenye uwezo wa kubeba risasi 100 katika chemba zake mbili za Kampuni ya Beta ('Century Magazines'), zilitumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume na dhidi ya polisi wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.”
Enock Maregesi