Å·±¦ÓéÀÖ

Sheria Quotes

Quotes tagged as "sheria" Showing 1-14 of 14
Enock Maregesi
“Jambazi aliyekubuhu hawezi kumuua mtu bila kumwambia kwa nini anamuua. Si sheria ya John Murphy. Ni sheria ya EAC.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kolonia Santita imesambaa dunia nzima. Hapa Meksiko wana magenge rafiki zaidi ya mia moja yakiwemo makubwa kabisa katika Latino ya Matamolos na Baja California. Nikitekwa nyara na memba yoyote wa magenge hayo, kuna uwezekano mkubwa wasinifanye chochote au nisilipe chochote kwa sababu ya Wanda. Fadhila ya uhalifu. Kwa sababu ya fadhila ya uhalifu; baba, au viongozi wengine wa serikali ambao watoto wao wamo ndani ya 'mpango' huo, wanatakiwa wawakingie kifua (kwa namna yoyote wanayoweza) pindi wanapoanguka katika mikono ya dola na sheria. Wasipofanya hivyo kutakuwa na vita ya ndani kwa ndani â€� kama unanielewa. Hivyo, kuna mtu anaitwa El Tigre â€� baba yake Wanda â€� ndiye ninayetaka unisaidie. Amemuua Marciano, na watu wengi wa Meksiko. Nataka kumlipia kisasi Marciano, na marafiki zangu wengi ambao El Tigre amewaua, hata kwa njia isiyodhahiri.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Hii ni sheria ya akili yangu: Akili yangu ni muhimu kuliko familia yangu. Nisipoitunza vizuri akili yangu, sitaitunza vizuri familia yangu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nje ya uwezo wa kisheria ni shetani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama nje ya uwezo wa kisheria ni uovu, hivyo basi, ndani ya uwezo wa kisheria ni wema. Kila mtu amepewa vipaji na Mwenyezi Mungu. Tumia vipaji vyako kutenda mema. Usitumie vipaji vyako kutenda maovu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuvunja sheria ni sawa na kufanya kosa, na kwa hiyo kuwa mkosaji, mbele ya sheria na mbele ya mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote. Serikali ya Meksiko ilipokataa kukidhi matakwa ya El Tigre ya kubadili katiba ya nchi â€� kuondoa kipengele cha mkataba wa kubadilishana watuhumiwa na washtakiwa â€� ili akikamatwa asipelekwe Marekani ambako atafungwa na kufia gerezani, El Tigre aliilaani Serikali ya Meksiko. Kujibu mapigo, ya laana ya maluuni, Serikali ya Meksiko ikawakabidhi makamanda 7 wa Kolonia Santita kwa mamlaka za Marekani, na kuongeza juhudi za kumsaka El Tigre mpaka nje ya Amerika ya Kusini na Kaskazini. El Tigre, kuikomoa serikali na kuwalipia kisasi makamanda wote waliouwawa na kufungwa na shirikisho, akamuua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (PGR) na maafisa 7 wa Jeshi la Polisi la Nchi (PJF) kulinganisha idadi ya makamanda wake waliopelekwa Marekani â€� halafu 'akapotea', kabisa; baada ya kutangaza vita na Serikali ya Meksiko!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Ukiwa na Yesu hutaishi kwa kutegemea rushwa, bali utaishi kwa kutegemea sheria. Ukiishi kwa kutegemea rushwa, rushwa itaishi kwa kukutegemea wewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kufanya kazi huku ukijua au hujui unavunja sheria ni uhuni. Sheria haina cha kujua au kutokujua sheria.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa) hawataweza kukutambua kwa sababu hujajisajili kwao, na kushirikiana na msanii ambaye hajajisajili BASATA ni kinyume cha sheria.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kujisajili ni lazima kwa mujibu wa sheria, lakini si kila msanii ambaye hajajisajili BASATA anajua kuwa anafanya kosa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kabla hawajakupiga kwa sheria wapige kwa kujisajili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Haki hushindana na sheria unapokuwa umeshtakiwa. Kama huna hatia lakini sheria ikasema una hatia, sheria imeishinda haki. Kama una hatia lakini sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria imeishinda haki. Kama huna hatia na sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria na haki vimelingana. Lakini kama utakata rufaa ikathibitika kwamba huna hatia, haki imeishinda sheria.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sheria wakati mwingine inaweza kuonea mtu. Pigana hata tone la mwisho kutetea haki yako.”
Enock Maregesi