Å·±¦ÓéÀÖ

Haki Quotes

Quotes tagged as "haki" Showing 1-12 of 12
Enock Maregesi
“Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mammon ni mungu wa pesa wa kuzimu anayesimamia mambo yote ya kifedha ulimwenguni. Ni miongoni mwa mashetani saba waliotupwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kutokea mbinguni akiwemo Ibilisi, Beelzebub, Asmodeus, Leviathan, Amon na Belphegor. Ibilisi ni mungu wa kiburi, Beelzebub ni mungu wa uroho, Asmodeus ni mungu wa zinaa, Leviathan ni mungu wa wivu, Amon ni mungu wa hasira na Belphegor ni mungu wa uvivu. Jukumu la mashetani hawa ni kusimamia kwa uaminifu mkubwa kutokea kuzimu dhambi kubwa saba duniani ambazo ni kiburi, uroho, zinaa, wivu, hasira, uvivu na uchoyo. Dawa ya dhambi hizo ni busara, kiasi, ujasiri, imani, haki, tumaini na upendo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa bendera ya taifa letu! Alikuwa alama ya amani, haki, uhuru, ujamaa, uzalendo, na Tanzania.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Jambo ambalo Mungu anataka tulitambue ni kwamba hatuko wenyewe katika bahari hii ya hewa. Hata nyangumi na wazira waovu wanapozunguka huko na huko baharini, ambao pia ni mapepo, wanaochukuliwa kama viumbe wabaya na wachafu na wala mizoga, wanaishi katika bahari hii ya hewa pamoja na sisi. Ni muhimu, kwa ajili ya ustawi wetu wa kiroho, kusikia onyo la Paulo katika Waefeso 6:10-12 kwamba vita yetu si dhidi ya hawa viumbe, na wanapambana usiku na mchana kutetea kile ambacho wanaamini ni cha kwao kwa sababu ya haki ya kuwepo hapa kwanza kabla yetu. Dunia, Biblia inatwambia, ilikuwa makazi yao ya kwanza (Yuda 1:6, KJV). Wanatuchukia kwa sababu taratibu tunakuwa Baba na Mwana, na kwa sababu wanajua hii dunia, urithi wetu, itachukuliwa kutoka mikononi mwao na kukabidhiwa kwa wale ambao ni watoto wa Mungu, wale ambao ni marafiki wa msalaba wa Yesu Kristo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Israeli ilifikia kikomo cha kipindi chake kikubwa cha mafanikio tangu enzi za Sulemani. Taifa lilikuwa tajiri. Lilikuwa na nguvu. Lilikuwa na silaha nyingi na nzuri zaidi. Lilikuwa taifa lililojidai kwa uwezo wake mkubwa wa nguvu za kijeshi, hekima, ujasiri, utajiri, na faida za kimkakati. Nani angeweza kushindana na Israeli? Lakini Mungu hunguruma onyo kwamba uwezo wote mkubwa wa asili wa taifa, ujuzi waliojipatia, na sifa bora zaidi havikuweza kulisaidia taifa la Israeli. Watu huona nguvu ya taifa katika utajiri wake, idadi yake ya watu, silaha za kijeshi, teknolojia, na maarifa. Lakini Mungu huangalia haki.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dhambi ikizidi katika taifa, Mungu ataliangamiza. Taifa likitenda haki, Mungu ataliinua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiongozi kwa sababu ya haki akibarikiwa na Mungu, hata watu anaowaongoza watabarikiwa na Mungu pia. Lakini kama kiongozi amelaaniwa na Mungu kwa sababu ya uovu, hata watu anaowaongoza watalaaniwa pia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Taifa ni malaika! Taifa ni Shetani! Laana ya mwenye haki ina haki.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Fidel Castro alitenda haki katika taifa lake ndiyo maana Mungu akamsaidia yeye na wananchi wake. Ijapokuwa ameondoka, lakini fikira zake sahihi zitaendelea kuwepo. Taifa la Kuba Mungu ataendelea kulibariki, kwa sababu fikira za Wakuba ni fikira za Fidel Castro.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna tofauti kati ya haki na utawala wa mabavu. Haki ni jambo ambalo mtu anastahili au kitu anachostahiki kuwa nacho. Utawala wa mabavu ni utawala wa kidikteta. Ukitenda haki lazima kuna watu watafaidi. Lazima kuna watu wataumia. Fidel Castro alikuwa kiongozi msahili. Alikuwa kiongozi aliyewezesha kutendeka kwa mambo. Kwa sababu hiyo, wachache walimpenda, wengi walimchukia. Lakini ili ufanye mazuri lazima upambane na mabaya. Shetani mwenyewe hatakuruhusu ufanye mazuri bila kukuletea mabaya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Haki hushindana na sheria unapokuwa umeshtakiwa. Kama huna hatia lakini sheria ikasema una hatia, sheria imeishinda haki. Kama una hatia lakini sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria imeishinda haki. Kama huna hatia na sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria na haki vimelingana. Lakini kama utakata rufaa ikathibitika kwamba huna hatia, haki imeishinda sheria.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Geuza hasira yako kuwa hasira ya Mungu ya haki.”
Enock Maregesi