ŷ

Dunia Nzima Quotes

Quotes tagged as "dunia-nzima" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Mpenzi. Sikiliza. Magaidi yaliyomuua Marciano yana mtandao dunia nzima na watu wote wanayajua. Yanaitwa Kolonia Santita. Tatizo hata hivyo ni moja: Hakuna mtu amewahi kuthibitisha au kutoa ushuhuda wa uhalifu wao ili watiwe nguvuni. Huendesha maisha yao kibabe na yana kila mbinu ya kukwepa sheria, ndani na nje ya Meksiko. Watu wengi wameuwawa kwa sababu ya Kolonia Santita. Ukileta kidomodomo yanakuua; au yanakupa notisi ya kuhama mji au nchi, ukakae mbali na Meksiko au Mexico City.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Saa nane za usiku timu nzima ya Vijana wa Tume ilirudi San Ángel katika helikopta ya DEA, tayari kwa safari ya Salina Cruz katika jimbo la Oaxaca. Kukamatwa kwa Gortari, Eduardo na Dongyang ulikuwa ushindi mkubwa wa kwanza wa Tume ya Dunia. Ushindi huo ukalipua wimbi la kukamatwa kwa wahalifu wa kimataifa, wa Kolonia Santita, dunia nzima.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kolonia Santita imesambaa dunia nzima. Hapa Meksiko wana magenge rafiki zaidi ya mia moja yakiwemo makubwa kabisa katika Latino ya Matamolos na Baja California. Nikitekwa nyara na memba yoyote wa magenge hayo, kuna uwezekano mkubwa wasinifanye chochote au nisilipe chochote kwa sababu ya Wanda. Fadhila ya uhalifu. Kwa sababu ya fadhila ya uhalifu; baba, au viongozi wengine wa serikali ambao watoto wao wamo ndani ya 'mpango' huo, wanatakiwa wawakingie kifua (kwa namna yoyote wanayoweza) pindi wanapoanguka katika mikono ya dola na sheria. Wasipofanya hivyo kutakuwa na vita ya ndani kwa ndani � kama unanielewa. Hivyo, kuna mtu anaitwa El Tigre � baba yake Wanda � ndiye ninayetaka unisaidie. Amemuua Marciano, na watu wengi wa Meksiko. Nataka kumlipia kisasi Marciano, na marafiki zangu wengi ambao El Tigre amewaua, hata kwa njia isiyodhahiri.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y. Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo, katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya Adamu, ambayo bado haijatakaswa. Damu ya Yesu si kitu kidogo. Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa. Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.”
Enock Maregesi

Auni Zainal
“Dunia tiba-tiba bagai sudah hilang warna. Setiap langkah kakinya hanya umpama daya luar yang mengheretnya untuk terus bergerak. Tidak ada apa-apa yang mengenyangkan. Tidak ada apa-apa yang melenakan.”
Auni Zainal, Mawaddah Ilmi Ingin Pulang