Seli Quotes
Quotes tagged as "seli"
Showing 1-4 of 4

“Kila sumu ina kiuasumu chake. Viuasumu vya 'cyanide' ni 'amyl nitrite', 'sodium nitrite', 'cyanokit', na 'sodium thiosulfate'. Kazi ya viuasumu hivi ni kuzalisha madini mengi ya chuma mwilini. Madini haya yatapambana na maada za rangi za uhai ('cytochromes') kwa ajili ya 'cyanide', ili 'cyanide' ing’ang’anie kwenye kiuasumu badala ya kung’ang’ania kwenye vimeng’enya vya seli za mwilini. Kiuasumu kinaposhinda mpambano huo; 'cyanide' hutolewa nje kwa njia ya mkojo, na mwathirika wa 'cyanide' hupona kabisa. 'Sodium thiosulfate' ndiyo bora zaidi kuliko 'amyl nitrite' au 'sodium nitrite', na ndiyo bora zaidi kuliko 'cyanokit'.”
―
―

“Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. Shetani asipokuona, utafanikiwa.”
―
―

“Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y. Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo, katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya Adamu, ambayo bado haijatakaswa. Damu ya Yesu si kitu kidogo. Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa. Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.”
―
―

“Kila binadamu ana nguvu ya ziada katika mwili wake ijulikanayo kitaalamu kama ATP. ATP (‘Adenosine Triphosphateâ€�) ni molekuli ndogo zaidi iliyoko ndani ya seli ambayo kazi yake ni kutengeneza nguvu ya ziada kwa ajili ya seli, na kwa ajili ya mwili mzima kwa jumla, pale mwili unapoonekana kukata tamaa au kuishiwa na nguvu kabisa. Ni kama jenereta ya umeme kwa ajili ya seli, inayofanya kazi pale umeme wa kawaida unapokatika.”
―
―
All Quotes
|
My Quotes
|
Add A Quote
Browse By Tag
- Love Quotes 99.5k
- Life Quotes 78k
- Inspirational Quotes 74.5k
- Humor Quotes 44.5k
- Philosophy Quotes 30.5k
- Inspirational Quotes Quotes 27.5k
- God Quotes 26.5k
- Truth Quotes 24k
- Wisdom Quotes 24k
- Romance Quotes 23.5k
- Poetry Quotes 22.5k
- Life Lessons Quotes 20.5k
- Death Quotes 20.5k
- Happiness Quotes 19k
- Quotes Quotes 18.5k
- Hope Quotes 18k
- Faith Quotes 18k
- Inspiration Quotes 17k
- Spirituality Quotes 15.5k
- Religion Quotes 15k
- Motivational Quotes 15k
- Writing Quotes 15k
- Relationships Quotes 15k
- Life Quotes Quotes 14.5k
- Love Quotes Quotes 14.5k
- Success Quotes 13.5k
- Time Quotes 12.5k
- Motivation Quotes 12.5k
- Science Quotes 12k
- Motivational Quotes Quotes 11.5k