Å·±¦ÓéÀÖ

Tunda Quotes

Quotes tagged as "tunda" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Mungu alimuumba mwanadamu ili aitawale dunia. Shetani tayari alikuwepo wakati Adamu anaumbwa. Adamu na Hawa walipokula tunda la mti wa katikati, walikufa kiroho â€� Yaani, walipoteza sura na asili ya Mungu â€� Shetani akawashinda kuanzia kipindi hicho na kuendelea. Tulizaliwa katika dhambi. Kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Njia pekee ya kuikomboa sura na asili ya Mungu ni kumpokea Yesu (Kristo) kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuwepo kwa Mti wa Uzima wa Milele katika Bustani ya Edeni (pamoja) na Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya inamaanisha, Adamu na Hawa walikuwa hai kiroho mpaka walipokula tunda la mti wa katikati ambapo hali yao ya maisha ilibadilika. Adamu na Hawa walikufa lakini hawakufa â€� walikufa baadaye kabisa. Hii inamaanisha kwamba (haya ni mawazo yangu tu) mtu anapokufa anakuwa amekula tunda la mti wa katikati, litakalomwezesha kuendelea kuishi katika hali nyingine ya maisha ambayo sisi hatuijui.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nini kingetokea kama Adamu na Hawa wasingekula tunda la Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya mpaka siku ya Sabato? Mungu angewaruhusu kula na lengo la uumbaji wa Mungu lingekamilika. Wanadamu wakifuata Amri Kumi za Mungu katika maisha yao watakuwa na uwezo maalumu ambao baadaye utawawezesha, kupitia Roho Mtakatifu, kuwa na maarifa ya siri ya uumbaji wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani ana mbinu nyingi za kuwateka wana wa Mungu. Mwanzo sura ya tatu inaonyesha jinsi Hawa alivyoona tunda linang’aa na akazama kwenye tunda pasipokujua kuna mauti ndani yake. Shetani anaangalia kipengele unachokitumia kuchukua maamuzi magumu naye anavaa jezi kama ya kwako ili usimgundue. Roho Mtakatifu akiwa anakuongoza penye hila nafsi yako itakuongoza.”
Enock Maregesi