欧宝娱乐

Wanadamu Quotes

Quotes tagged as "wanadamu" Showing 1-14 of 14
Enock Maregesi
“Hasira ni Shetani. Hekima ni Mungu. Kila kitu kimo ndani yetu. Hasira imo ndani yetu. Hekima imo ndani yetu. Atomu ni matofali ya ujenzi wa kila kitu ulimwenguni likiwemo jua na miili ya wanadamu. Ndani ya atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi. Kama miili yetu imetengenezwa na atomu na katika kila atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi, hivyo basi, tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mazuri na tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mabaya. Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana. Geuza hasira yako kuwa hekima kwa faida yako na kwa faida ya wengine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ni ya muhimu kwa sababu ya mahitaji ya lazima ya wanadamu kama vile chakula, maji, malazi, elimu, usafi, mavazi, na afya, lakini ni ya maana kwa sababu ya wanawake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wengine hatuishi kama wafalme kwa sababu ya nguvu za giza 鈥� zilizopo kati ya Mungu na wanadamu. Nyota zetu zimefunikwa. Una kila kitu unachotafuta, ndani ya moyo wako. Usitafute furaha, utajiri au amani nje ya moyo wako. Tafuta furaha, utajiri au amani ndani ya moyo wako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nini kingetokea kama Adamu na Hawa wasingekula tunda la Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya mpaka siku ya Sabato? Mungu angewaruhusu kula na lengo la uumbaji wa Mungu lingekamilika. Wanadamu wakifuata Amri Kumi za Mungu katika maisha yao watakuwa na uwezo maalumu ambao baadaye utawawezesha, kupitia Roho Mtakatifu, kuwa na maarifa ya siri ya uumbaji wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi wanamwabudu Shetani. Lakini Shetani wanayemwabudu si Shetani Ibilisi aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu kuja kuudanganya ulimwengu wote. Ni Shetani roho ya mabadiliko, mabadiliko ya kweli, ya ufahamu kamilia ulimwengu huu ambamo sisi sote tunaishi. Wachawi, kwa maneno mengine, wanaabudu miungu 鈥� kama vile Inanna wa Mesopotamia, Isis wa Misri, Asherah wa Kaanani au Belus wa Assyria ambaye ndiye mungu wa kwanza kuabuadiwa kama sanamu duniani 鈥� iliyotwaliwa na Shetani tangu misingi ya ulimwengu huu kusimikwa. Dhambi aliyotenda Shetani mbinguni ni ndogo kuliko dhambi wanazotenda wachawi duniani, ijapokuwa dhambi aliyotenda Shetani haitaweza kusamehewa na ndiyo maana Shetani hataweza kuwasamehe wanadamu. Ni jukumu letu kuwaita wachawi wote kutoka Babeli na kuwaleta katika ukweli kama kweli wanayemwabudu ni Shetani Ibilisi, Shetani Beelzebub, Shetani Asmodeus, Shetani Leviathan, Shetani Mammon, Shetani Amon au Shetani Belphegor ambao ni mabingwa wa kiburi, uroho, zinaa, wivu, fedha, hasira na uvivu duniani. Wachawi hawajui, na usipojua waweza kufa bila kujua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hawezi kusoma ndani ya mioyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Ukionyesha tamaa ya chuki, Shetani atakupa chuki. Ukionyesha tamaa ya upendo, Mungu atakupa upendo. Kama kuna ubishi kati ya moyo wako na akili yako, fuata moyo wako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kwa vile hatasamehewa, Shetani hatawasamehe wanadamu. Atahakikisha anauwa kila mtu duniani na kumpeleka kuzimu; ambako anaishi yeye, majini, malaika waovu, wana wa Mungu waliotumwa na Mungu kuja duniani kufundisha watu utukufu lakini wakaasi na Mungu akawalaani (au Wanefili) pamoja na nguva. Nguva ni uzao wa Wanefili na samaki wa baharini na malaika wauvu na wanapatikana zaidi katika Bahari ya Atlantiki, ambako mkuu wake ni Malkia wa Pwani, na katika Bahari ya Hindi ambako mkuu wake ni Malkia wa Bahari ya Hindi. Chini ya Bahari ya Hindi ndipo yalipo makao makuu ya ufalme wa giza hapa duniani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. Shetani asipokuona, utafanikiwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu 鈥� na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kabla ya uasi, Mungu alimpa Shetani na wasaidizi wake ambao ni mapepo mamlaka makubwa juu ya kila kitu hapa duniani; kuanzia angahewa la dunia hadi ardhi ya dunia nzima nasi wakazi wake tukijumuishwa. Abadani tusisahau kwamba, kwa kiasi kikubwa, kupambana kwetu kama Paulo anavyosema ni dhidi ya hawa mapepo na mfalme wao ambaye ni Shetani. Tunaishi katika eneo ambapo hata wao wanaishi.

Hawa mapepo wabaya huwatumia maadui wa msalaba wa Yesu Kristo kutekeleza mipango yao kwa lengo la kuwaangamiza marafiki wote wa msalaba wa Yesu Kristo, wanashawishiwa kwa kiasi kikubwa na hizo mamlaka za kimapepo, na kwa sababu wamedanganywa, hawajui hata kidogo kama Shetani anawatumia! Inawezekana hawajatwaliwa na mapepo lakini wanashawishiwa na mapepo kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu kwa wanadamu wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hatawasamehe wanadamu kwa sababu ya kiburi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mtu anayejaribu kupambana na Mungu anajaribu kupambana na jambo lisilowezekana. Hatakuwa na uwezo wa kushinda. Kufanya hivyo ni upumbavu usioweza kuelezeka, lakini wanadamu hatukomi kufanya hivyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hawezi kusoma ndani ya myoyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Usimpe nafasi Shetani.”
Enock Maregesi