Å·±¦ÓéÀÖ

Maarifa Quotes

Quotes tagged as "maarifa" Showing 1-19 of 19
Enock Maregesi
“Kwa sababu ya udadisi wa hali ya juu nasoma kila kitu ninachokutana nacho hasa vile visivyonipendeza. Ukitaka kupata maarifa usisome tu vitabu vinavyokupendeza. Soma vitabu visivyokupendeza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nilijifunza toka awali umuhimu wa kushindwa katika maisha ijapokuwa nilijitahidi sana, na nilipoendelea kushindwa niliweka nadhiri ya kufanya kitu kimoja kilicholeta maana zaidi katika maisha yangu nacho ni uandishi wa vitabu. Uandishi wa vitabu ndicho kitu pekee nilichokiweza zaidi kuliko vingine vyote na kuanzia hapo Mungu aliniweka huru. Nilijua mimi ni nani. Nilijua kwa nini nilizaliwa. Nilijifunza falsafa ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko nilivyoikuta â€� kwa sababu hata mimi nilikuwepo â€� na falsafa ya kushindwa si hiari. Maarifa hayo yakafanya niwe na heshima na upendo kwa watu wote.”
Enock Maregesi

Lao Tzu
“kuwajua wengine ni hekima, kujijua mwenyewe ni maarifa makubwa”
Lao Tzu

Enock Maregesi
“Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nini kingetokea kama Adamu na Hawa wasingekula tunda la Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya mpaka siku ya Sabato? Mungu angewaruhusu kula na lengo la uumbaji wa Mungu lingekamilika. Wanadamu wakifuata Amri Kumi za Mungu katika maisha yao watakuwa na uwezo maalumu ambao baadaye utawawezesha, kupitia Roho Mtakatifu, kuwa na maarifa ya siri ya uumbaji wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu anapokupa kipaji anategemea ukitumie vizuri kwa ajili ya wengine. Usipokitumia vizuri kwa ajili ya wengine, ama kwa uvivu au kwa woga, atawapa wengine wakitumia kwa ajili yako. Ukitumia vipaji vyako vizuri, Mungu atakuongezea maradufu. Yaani, ukitumia muda wako vizuri atakuongezea muda. Ukitumia nguvu zako vizuri atakuongea nguvu. Ukitumia pesa yako vizuri atakuongezea pesa. Ukitumia ukarimu wako vizuri atakuongezea ukarimu. Ukitumia maarifa yako vizuri atakuongezea maarifa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maarifa unayoyatafuta katika Biblia, Kurani au Yoga ('Oriental Yoga': 'esoteric knowledge': maarifa ya kujua siri ya uumbaji wa Mungu ya 'Kabbalah' ya Kiyahudi au 'Kalachakra' ya Kibudha ya bara la Asia; siri ya sayansi ya kurefusha maisha ya mafundisho ya kiroho ya 'Arcanum' ya Misri â€� au Kemia ya Mungu au 'Alchemy'; mafundisho ya kiroho ya 'Rosicrucia' ya bara la Ulaya tangu mwishoni mwa karne ya kumi na nne; 'sex magic', 'sex magic' inaweza kukupa utajiri au umaskini hivyo kuwa makini; n.k.) ni hekima na busara. Vingine vyote vitajileta vyenyewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi hivi ndivyo wanavyoapishwa na kuikana imani ya Kikristo: Mwanafunzi hupelekwa kilingeni katika siku maalumu kuonana na Shetani, pamoja na jopo la wachawi. Shetani hutokea katika mwili wa hewa, mwili uliochanganyikana na hewa na mvuke mzito, wa mwanamume na kuwasihi waishikilie imani yao kwake kwa mioyo yao yote, huku akiwaahidi utajiri na maisha marefu kama hawatamkana. Kisha wachawi wanampendekeza mwanafunzi kwa Shetani. Shetani humuuliza mwanafunzi kama yuko tayari kuikana imani yake, kuachana na Ukristo na kutokumwabudu Mwanamke Aliyebarikiwa Kuliko Wanawake Wote Duniani Maria Magdalena, na kutoziheshimu sakaramenti za aina zote. Mwanafunzi atakapokubaliana na masharti hayo, Shetani atanyoosha mkono wake na kumsihi mwanafunzi anyooshe wa kwake. Kwa mkono wake mwenyewe, mwanafunzi ataapa na kuweka agano na Shetani mbele ya jopo la wachawi.

Baada ya hapo bila kuchelewa Shetani ataendelea na kusema kuwa hicho kiapo hakitoshi. Lakini mwanafunzi atakapouliza afanye kitu gani cha ziada, Shetani atahitaji kiapo kifuatacho kwa heshima yake na kwa heshima ya mashetani wote: Mwanafunzi ajikabidhi kwa Shetani kwa mwili na kwa roho yake yote daima dawamu, na afanye kila awezalo kuleta wanafunzi wengine wa kike na wa kiume katika ufalme wake. Kama hiyo haitoshi Shetani ataongeza kuwa lazima mwanafunzi atengeneze mafuta fulani kutokana na mifupa na viungo vya miili ya watoto, hasa watoto waliobatizwa, kwani kwa kufanya hivyo atamtimizia kila kitu atakachokitaka hapa duniani. Hiyo ni njia mojawapo ya kiapo.

Njia nyingine ya kiapo ni kwa wale ambao hawajiamini au wana hofu ya kuonana na Shetani uso kwa uso kilingeni, akiwa na mwili wa kimazingaombwe na sauti ya kutisha kwani Shetani hana mapafu wala hana ulimi. Badala ya kilingeni mwanafunzi hupelekwa kanisani na jopo la wachawi ambapo mbele ya jopo atalazimishwa kuikana imani yake, kumkana Yesu Kristo, kuukana ubatizo na kulikana kanisa zima kwa ujumla wake. Mwanafunzi baada ya hapo atalazimishwa kutoa heshima kuu kwa Mfalme Mdogo, kwani hivyo ndivyo wanavyomwita Shetani ili kumwondolea mwanafunzi hofu, kisha atalazimishwa kunywa supu ya mtoto mchanga waliyemuua akazikwa kisha wakamfukua na kupika viungo vya mwili wake; na dakika hiyo mwanafunzi atapata maarifa, maarifa ya kichawi, kama walimu wake na watarudi nyumbani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini kuna ndoto takatifu na kuna ndoto za kishetani. Ndoto takatifu hutokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika, kama ambavyo usiku unavyokuwa kimya na kila kitu kimetulia, karibu na saa za alfajiri, ambapo mfumo wa usagaji chakula unakuwa umemaliza kazi yake. Kipindi hicho malaika wa Mungu hutufunulia siri kuhusu ulimwengu huu, ili kwamba tutakapoamka asubuhi tuwe na baadhi ya maarifa yaliyojificha ndani ya maandiko ya vitabu vitakatifu; kwa sababu malaika wa Mungu ndiye anayetawala ufahamu wetu, kama ambavyo Mungu anavyotawala hiari yetu, na kama ambavyo nyota zinavyotawala miili yetu. Lakini kwa wale waliokomaa kiimani malaika mwema anaweza kuwafunulia siri wakati wowote, haijalishi wamelala au wameamka. Kwa ajili ya ujanja wa Shetani ndiyo maana Mungu hutufunulia siri zake, ili tujihadhari naye.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ndiye aliyetengeneza ubongo. Ni vizuri kuamini kwamba Yeye ndiye anayetupa maarifa, kupitia malaika wema, kuhusu maisha yetu na kuhusu siri ya uumbaji wake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wanaamini kuwa Yesu atarudi tarehe 29 Julai 2016. Tarehe hiyo kitu kikubwa sana kitatokea katika dunia yetu kitakachosababisha tetemeko kubwa la ardhi, litakalosababishwa na kubadilika kwa ncha za dunia, tendo litakalosababisha mionzi ya gama kutoka kwenye jua ifike duniani na kuua kila kitu kinachoonekana katika uso wa dunia hii. Watakatifu watafufuka na kumlaki Kristo mawinguni, ambaye anakuja kuwachukua wateule na kumweka Shetani kifungoni kwa miaka 1000. Hayo yote, wanasema, yatatokea ndani ya siku 11 kuanzia leo. Yaani, kusini mwa dunia kutakuwa kaskazini mwa dunia, kaskazini mwa dunia kutakuwa kusini mwa dunia.

Kitendo hicho kitafanya dunia ikose kinga ya sumaku iitwayo ‘magnetosphereâ€� ambayo hukinga dunia dhidi ya mionzi ya gama kutoka kwenye jua. Mionzi hiyo hugonga ukuta wa ‘magnetosphereâ€� kila baada ya dakika 8 kwa mwendokasi wa kilometa milioni 1080 kwa saa; na kusambazwa katika ncha za dunia ambapo aghalabu huchanganyikana na oksijeni na kutengeneza kitu kinaitwa ‘auroraâ€�, au mwanga wa ncha, ambacho ni maajabu mengine ya angani. Mwaka 2012 wanasayansi walisema ncha za dunia zingebadilika lakini hazikubadilika. Je, muda umefika sasa wa kuwaamini wanasayansi? Biblia ni chuo cha Mungu. Soma Biblia kupata maarifa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwa karibu na Mungu utakuwa na maarifa kuliko profesa, Mungu ana maarifa kuliko profesa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usipofanya kazi kwa bidii na maarifa utaendelea kuuliza Mbagala tupande daladala gani, badala ya kuuliza Mbagala tupite njia gani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maarifa ni mbegu ya mabadiliko.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maarifa hupunguza woga.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wengi hawana maarifa kwa sababu ya elimu na utajiri. Hawana elimu na hawana utajiri. Nchi iwape wananchi wake kila kitu isipokuwa ujinga na umaskini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna siri nyingi za ndani zinazofanya mtu aendelee kufanikiwa, na kuna siri nyingi za nje zinazofanya mtu aendelee kuficha siri ya mafanikio yake. Siri za ndani ni siri za kweli, ilhali siri za nje ni siri za uongo, zenye lengo la kuficha ukweli. Hata hivyo, siri ya mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, pamoja na siri.”
Enock Maregesi