Å·±¦ÓéÀÖ

Upendeleo Quotes

Quotes tagged as "upendeleo" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Upendeleo na msamaha ni sumu na baraka ya usuluhishi miongoni mwa watu kwa mpangilio huo. Yaani, upendeleo ni sumu ya usuluhishi, msamaha ni baraka ya usuluhishi. Usuluhishi wenye msamaha, usiokuwa na upendeleo wowote, ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu. Upendeleo ni sumu ya usuluhishi â€� Msamaha ni kiuasumu cha usuluhishi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna nguzo saba ambazo hazina budi kuzingatiwa kama unataka kuheshimiwa na kuwaheshimu wengine. Kwanza kabisa jitambue: wewe ni nani na unafanya nini hapa duniani. Halafu, kabla ya kusema jambo lolote kwa mtu yoyote fikiria kwanza maana au madhara ya hilo unalotaka kulisema. Kisha jifunze tamaduni mbalimbali na watendee wengine kama vile unavyotaka kutendewa au kama vile wanavyotaka kutendewa. Jifunze kusamehe na kusuluhisha migogoro katika jamii unamoishi huku ukidumisha heshima na utu kwa binadamu wenzako. Jijengee imani kwa watu, punguza upendeleo, fanya kazi kama timu kwani hakuna ‘mimiâ€� katika umoja ila kuna ‘sisiâ€�, na jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE kwa manufaa ya wote. Kuwa kiongozi katika kila jambo unalofanya na katika kila kitu unachofanya. Jitahidi kufanya jambo au kitu kwa usahihi kwa kadiri utakavyoweza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kwa vile taifa la Israeli lilipoteza haki yake ya upendeleo, Mungu aliahidi kuliharibu kama alivyoyaharibu mataifa ya Waamori na Wamisri. Watu wa Israeli walishafika mbali sana kiasi cha Mungu kutokutegemea tena toba kutoka kwao. Kuna muda wa fursa na kuna muda ambao fursa haipo tena. Nafasi ya Israeli ya kutubu ilishafikia mwisho.

Kama alivyokuwa amepigana vita vyao kwa ajili yao katika siku za nyuma sasa Mungu alipigana nao. Pamoja na ujasiri na utaalamu wao wote wasingependelewa tena. Mambo ambayo mwanzo yaliipa Israeli nguvu katika vita yaliwageukia.”
Enock Maregesi