Å·±¦ÓéÀÖ

Sumu Quotes

Quotes tagged as "sumu" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya 'hydrogen cyanide'. Gesi ya 'hydrogen cyanide' ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha 'cyanide' atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi â€� kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote â€� hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Upendeleo na msamaha ni sumu na baraka ya usuluhishi miongoni mwa watu kwa mpangilio huo. Yaani, upendeleo ni sumu ya usuluhishi, msamaha ni baraka ya usuluhishi. Usuluhishi wenye msamaha, usiokuwa na upendeleo wowote, ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu. Upendeleo ni sumu ya usuluhishi â€� Msamaha ni kiuasumu cha usuluhishi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kila sumu ina kiuasumu chake. Viuasumu vya 'cyanide' ni 'amyl nitrite', 'sodium nitrite', 'cyanokit', na 'sodium thiosulfate'. Kazi ya viuasumu hivi ni kuzalisha madini mengi ya chuma mwilini. Madini haya yatapambana na maada za rangi za uhai ('cytochromes') kwa ajili ya 'cyanide', ili 'cyanide' ing’ang’anie kwenye kiuasumu badala ya kung’ang’ania kwenye vimeng’enya vya seli za mwilini. Kiuasumu kinaposhinda mpambano huo; 'cyanide' hutolewa nje kwa njia ya mkojo, na mwathirika wa 'cyanide' hupona kabisa. 'Sodium thiosulfate' ndiyo bora zaidi kuliko 'amyl nitrite' au 'sodium nitrite', na ndiyo bora zaidi kuliko 'cyanokit'.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Msamaha si jambo dogo. Watu wadogo, watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri, hawawezi kupambana na changamoto za msamaha. Msamaha ni kwa ajili ya watu wenye macho kama ya tai wanaoweza kuona mbali ambao wako tayari kushindwa vita ili washinde vita. Hewa inaingia ndani ya mapafu na kutoka; chakula kinaingia ndani ya mwili na kutoka; mwanamasumbwi anapigana bila kugombana; injini ya gari haiwezi kusukuma gari mbele au nyuma bila kutoa hewa katika paipu ya ekzosi. Lakini kile kinachoingia moyoni mwako hakitoki! Maumivu yanapoingia ndani ya moyo yanapaswa kutoka nje kama yalivyoingia kwa sababu, yasipotoka yatatengeneza sumu ndani ya moyo wako na yatatengeneza sumu ndani ya roho yako pia. Sumu hiyo itahatarisha safari yako ya mbinguni na Mungu hatakusamehe tena. Badala ya yule aliyekukosea kuumia, utaumia wewe uliyekosewa. Yesu anaposema samehe saba mara sabini hatanii. Usiposamehe, hutasamehewa.”
Enock Maregesi