Msamaha Quotes
Quotes tagged as "msamaha"
Showing 1-17 of 17

“Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.”
―
―

“Kama umefanya au umesema kitu kibaya na ukasema ukweli mbele ya mtu au ya watu, omba msamaha kupata tena kibali cha umma.”
―
―

“Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka wazi kwamba unapomsamehe mtu, huwezi kupotezea au kukana uzito wa kosa alilokufanyia. Kusamehe ni hali fulani inayotoka ndani ya moyo wa mtu, ikiwa na hali ya uhuru wa hiari wa mtu mwenyewe kuamua kuachilia kile kinachomuumiza, pasipo kuwepo masharti ya aina yoyote ile kwa mtu aliyemuumiza.”
―
―

“Upendeleo na msamaha ni sumu na baraka ya usuluhishi miongoni mwa watu kwa mpangilio huo. Yaani, upendeleo ni sumu ya usuluhishi, msamaha ni baraka ya usuluhishi. Usuluhishi wenye msamaha, usiokuwa na upendeleo wowote, ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu. Upendeleo ni sumu ya usuluhishi â€� Msamaha ni kiuasumu cha usuluhishi.”
―
―

“Msamaha si jambo rahisi. Tunapoumizwa, au watu wetu wa karibu wanapoumizwa, tendo la kusamehe linaweza kuwa gumu kuliko matendo yote. Lakini, tambua kwamba msamaha ni mchakato wa muda mrefu unaohitaji ujasiri mkubwa kuuanza hadi kuukamilisha, ongea na watu wanaoelewa maana ya msamaha ili wakuongoze katika mchakato huo. Vilevile, tambua kwamba hata wewe umewahi kufanya makosa na unahitaji msamaha, tambua kwamba suluhisho kamili linahitaji matendo kutoka kwa aliyekosea na kwa aliyekosewa. Wengine hupendwa kwa sababu wanastahili, lakini wengine wanastahili kwa sababu hupendwa. Mungu anatupenda kwa jinsi tulivyo hata kama tunajiona hatustahili. Hivyo, jithamini.”
―
―

“Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.”
―
―

“Msamaha si kwa ajili ya watu wenye mabawa ya kuku, ni kwa ajili ya watu wenye macho ya tai. Kua kuujua msamaha.”
―
―

“Msamaha si jambo dogo. Watu wadogo, watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri, hawawezi kupambana na changamoto za msamaha. Msamaha ni kwa ajili ya watu wenye macho kama ya tai wanaoweza kuona mbali ambao wako tayari kushindwa vita ili washinde vita. Hewa inaingia ndani ya mapafu na kutoka; chakula kinaingia ndani ya mwili na kutoka; mwanamasumbwi anapigana bila kugombana; injini ya gari haiwezi kusukuma gari mbele au nyuma bila kutoa hewa katika paipu ya ekzosi. Lakini kile kinachoingia moyoni mwako hakitoki! Maumivu yanapoingia ndani ya moyo yanapaswa kutoka nje kama yalivyoingia kwa sababu, yasipotoka yatatengeneza sumu ndani ya moyo wako na yatatengeneza sumu ndani ya roho yako pia. Sumu hiyo itahatarisha safari yako ya mbinguni na Mungu hatakusamehe tena. Badala ya yule aliyekukosea kuumia, utaumia wewe uliyekosewa. Yesu anaposema samehe saba mara sabini hatanii. Usiposamehe, hutasamehewa.”
―
―

“Yesu alipokuwa msalabani watu wengi walimzunguka. Askari wa Kirumi aliyekuwa na chongo, na mkuki, alikuwa na jukumu la kumtesa Yesu hadi kufa kwa amri ya Pilato. Yesu alipolia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?â€�, yule askari alikurupuka na kumwendea Yesu. Lakini Yesu alishakata roho. Kuthibitisha kama Yesu alishakata roho, askari alimchoma Yesu mkuki kwenye mbavu kwa nguvu zake zote. Mkuki huo ukamtoboa Yesu hadi upande wa pili, ukatoboa hata moyo wake. Askari alipochomoa mkuki, damu na maji viliruka na kupiga jicho lake bovu. Papo hapo askari akapona na kuona vizuri. Alipoona kweli amepona na kuona vizuri, askari alipiga kelele, alipiga magoti na kuomba Mungu amsamehe dhambi zake. Msamaha una nguvu kuliko dhambi. Askari huyo atakwenda mbinguni. Haijalishi umechukia watu kiasi gani. Haijalishi umetesa watu kiasi gani. Haijalishi umeua watu kiasi gani. Haijalishi umetenda dhambi kiasi gani. Mungu anachotaka kutoka kwako, tubu.”
―
―

“Toa msamaha usiokuwa na masharti yoyote kwa yeyote aliyekukosea kwa sababu, dhambi iliyofanya mkosane ilitoka kwa Shetani. Kwa mfano, usiseme umesamehe lakini hutasahau, sema umesamehe na umesahau.”
―
―

“Mbegu ni neno la Mungu. Mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni maneno ya Mungu. Kwa hiyo mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni mbegu. Watu ni ardhi. Panda mbegu ya mfano bora kwa watoto wako, msamaha kwa maadui zako, ndoto kwa malengo yako, tabasamu kwa marafiki zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli, uchapakazi kwa kazi zako na uvumilivu kwa wapinzani wako. Kila mbegu irutubishwe kwa imani na upendo kwa watu.”
―
―

“Mbegu ni neno la Mungu. Mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni maneno ya Mungu. Kwa hiyo mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni mbegu. Watu ni ardhi. Panda mbegu ya mfano bora kwa watoto wako, msamaha kwa maadui zako, ndoto kwa malengo yako, tabasamu kwa marafiki zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli, uchapakazi kwa kazi zako na uvumilivu kwa wapinzani wako. Kila mbegu irutubishwe kwa imani na upendo kwa watu.
Katika mfano huu ukuaji unawakilisha utakaso, ambao ni muundo wa taswira ya Mungu ndani yetu kwa kuishi kama anavyoishi yeye kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Tunachotakiwa kufanya baada ya kupanda mbegu ni kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe ni sawa na mvua, jua, palizi, mbolea, ili mavuno yaweze kuwa ya uhakika.”
―
Katika mfano huu ukuaji unawakilisha utakaso, ambao ni muundo wa taswira ya Mungu ndani yetu kwa kuishi kama anavyoishi yeye kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Tunachotakiwa kufanya baada ya kupanda mbegu ni kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe ni sawa na mvua, jua, palizi, mbolea, ili mavuno yaweze kuwa ya uhakika.”
―
All Quotes
|
My Quotes
|
Add A Quote
Browse By Tag
- Love Quotes 99.5k
- Life Quotes 78k
- Inspirational Quotes 74.5k
- Humor Quotes 44.5k
- Philosophy Quotes 30.5k
- Inspirational Quotes Quotes 27.5k
- God Quotes 26.5k
- Truth Quotes 24k
- Wisdom Quotes 24k
- Romance Quotes 23.5k
- Poetry Quotes 22.5k
- Life Lessons Quotes 20.5k
- Death Quotes 20.5k
- Happiness Quotes 19k
- Quotes Quotes 18.5k
- Hope Quotes 18k
- Faith Quotes 18k
- Inspiration Quotes 17k
- Spirituality Quotes 15.5k
- Religion Quotes 15k
- Motivational Quotes 15k
- Writing Quotes 15k
- Relationships Quotes 15k
- Life Quotes Quotes 14.5k
- Love Quotes Quotes 14.5k
- Success Quotes 13.5k
- Time Quotes 12.5k
- Motivation Quotes 12.5k
- Science Quotes 12k
- Motivational Quotes Quotes 11.5k