欧宝娱乐

Wote Quotes

Quotes tagged as "wote" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“ATP hutumika katika kipindi ambapo mtu anakuwa amekata tamaa kabisa katika jambo lolote analolifanya, na yeyote anayetumia ATP ana uwezo mkubwa wa kufanikiwa katika maisha yake. Hivyo, usikate tamaa, jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna nguzo saba ambazo hazina budi kuzingatiwa kama unataka kuheshimiwa na kuwaheshimu wengine. Kwanza kabisa jitambue: wewe ni nani na unafanya nini hapa duniani. Halafu, kabla ya kusema jambo lolote kwa mtu yoyote fikiria kwanza maana au madhara ya hilo unalotaka kulisema. Kisha jifunze tamaduni mbalimbali na watendee wengine kama vile unavyotaka kutendewa au kama vile wanavyotaka kutendewa. Jifunze kusamehe na kusuluhisha migogoro katika jamii unamoishi huku ukidumisha heshima na utu kwa binadamu wenzako. Jijengee imani kwa watu, punguza upendeleo, fanya kazi kama timu kwani hakuna 鈥榤imi鈥� katika umoja ila kuna 鈥榮isi鈥�, na jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE kwa manufaa ya wote. Kuwa kiongozi katika kila jambo unalofanya na katika kila kitu unachofanya. Jitahidi kufanya jambo au kitu kwa usahihi kwa kadiri utakavyoweza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Boresha maisha ya watu kwa kadiri utakavyoweza. Ukisaidia mtu 1 watahurumiwa watu 10. Ukisaidia watu 10 watahurumiwa watu 100. Ukisaidia watu 100 watahurumiwa watu 1000. Kila mmoja wetu akitambua wajibu wake katika jamii, Mungu atatuhurumia sisi wote. Maisha ya mtu mmoja yakiboreka, mmoja huyo ataboresha na ya wengine wengi. Hivyo, endelea kuogelea lakini usisahau kurudi nyuma katika jamii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukila chakula mwili wote unafaidi! Ukiomba kitu kwa Mungu omba kwa ajili ya wote.”
Enock Maregesi