Maombi Quotes
Quotes tagged as "maombi"
Showing 1-11 of 11

“Ijapokuwa maombi ya sifa yana nguvu kuliko maombi ya kushukuru, kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba.”
―
―

“Maombi ya sifa huunganisha watu wa Mungu na hutayarisha njia kwa ajili ya uwezo wa Mungu katika maisha yetu. Thamani ya maombi ya sifa wakati wa matatizo ni kuimarisha imani yetu, na kuwa karibu na Mungu wetu. Mungu anataka tumpe sifa na kumshukuru kwa kila jambo, kama Mtume Paulo anavyosema katika waraka wa kwanza wa Wathesalonike 5:16-18. Kumshukuru Mungu wakati wa matatizo ni amri, si ombi.”
―
―

“Binti yako mwenye umri wa miaka kumi na nne kwa mfano, anaomba umnunulie gari kama ulivyofanya kwa kaka yake mwenye umri wa miaka kumi na nane. Mara ya kwanza unamwambia utamnunulia atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane kama ulivyofanya kwa kaka yake. Lakini baada ya wiki moja binti yako anakuomba tena kitu kilekile, yaani gari. Utajisikiaje? Utakereka, sivyo? Jinsi utakavyokereka binti yako kukuomba kitu ambacho tayari ameshakuomba, ndivyo Mungu anavyokereka sisi kumwomba vitu ambavyo tayari tumeshamwomba. Ukiomba kitu kwa mara ya kwanza Mungu amekusikia, tayari ameshaandaa malaika wa kukuletea jibu. Unachotakiwa kufanya, baada ya kuomba, shukuru mpaka jibu lako litakapofika. Mungu huthamini zaidi maombi ya kushukuru kuliko maombi ya kuomba. Binti yako anachotakiwa kufanya baada ya kukuomba gari ni kukushukuru mpaka gari yake itakapofika, si kukuomba mpaka gari yake itakapofika.”
―
―

“Mtu akikutukana mwambie asante au samahani. Asante au samahani vina nguvu kuliko kuomba (asikutukane) au kutukana.”
―
―

“Nguvu za hasi ni mawazo mabaya, na nguvu za chanya ni mawazo mazuri. Nguvu za hasi ni Shetani, kwa vile Shetani ndiye anayeleta mabaya. Nguvu za chanya ni Mungu, kwa vile Mungu ndiye anayeleta mazuri. Katika dunia hii utapambana na Shetani lakini hutamshinda, kwani hapa ndipo anapotawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho, kwa maana ya maombi na utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu, kama unataka kuzishinda nguvu zake.”
―
―

“Kiungo chochote kikikuuma ghafla na kuacha au kikiendelea kukuuma kwa muda fulani halafu kikaacha, halafu huna sababu ya kwa nini kinakuuma, angalia unawaza nini wakati kiungo hicho kinakuuma. Kisha lifanyie kazi wazo hilo kwa maombi hata ya sekunde tano! Funika tatizo hilo, hata kama hulijui, kwa damu ya Yesu!”
―
―

“Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. Shetani asipokuona, utafanikiwa.”
―
―

“Damu ya Mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi. Mungu hauwi, Anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Ukifunikwa na damu ya Mwanakondoo Shetani, ambaye ni wakala, hatakuona. Lakini Mungu atakuona. Bila kafara ya damu hakuna msamaha wa dhambi. Bila kafara ya damu hakuna mafanikio.”
―
―

“Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu â€� na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.”
―
―
All Quotes
|
My Quotes
|
Add A Quote
Browse By Tag
- Love Quotes 99.5k
- Life Quotes 78k
- Inspirational Quotes 74.5k
- Humor Quotes 44.5k
- Philosophy Quotes 30.5k
- Inspirational Quotes Quotes 27.5k
- God Quotes 26.5k
- Truth Quotes 24k
- Wisdom Quotes 24k
- Romance Quotes 23.5k
- Poetry Quotes 22.5k
- Life Lessons Quotes 20.5k
- Death Quotes 20.5k
- Happiness Quotes 19k
- Quotes Quotes 18.5k
- Hope Quotes 18k
- Faith Quotes 18k
- Inspiration Quotes 17k
- Spirituality Quotes 15.5k
- Religion Quotes 15k
- Motivational Quotes 15k
- Writing Quotes 15k
- Relationships Quotes 15k
- Life Quotes Quotes 14.5k
- Love Quotes Quotes 14.5k
- Success Quotes 13.5k
- Time Quotes 12.5k
- Motivation Quotes 12.5k
- Science Quotes 12k
- Motivational Quotes Quotes 11.5k