Å·±¦ÓéÀÖ

Udongo Quotes

Quotes tagged as "udongo" Showing 1-6 of 6
Enock Maregesi
“Nyota ni kipaji, kipawa, takdiri, karama, au uweza; ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu, au takdiri ya maisha ya mwanadamu. Unabii na nyota ya ufalme ni kibali cha Mungu katika maisha ya mtu. Kupata kibali hicho, tembea na watu sahihi katika maisha yako (tembea na watu ambao Mungu amekuchagulia kushika funguo za takdiri ya maisha yako). Tamka na kukiri kibali cha Mungu katika maisha yako yote. Panda mbegu za kibali cha Mungu katika udongo wa maisha yako. Jifunze kutenda mema bila malipo, kwani wema ni mbegu ya kibali cha Mungu. Jali mambo ya ufalme wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Roho haina mifumo ya ufahamu! Haina pua, haina macho, haina ladha, haina harufu wala haina masikio. Kwa sababu roho haina mifumo ya ufahamu mtu, anapokufa mifumo yake yote 21 aliyokuwa nayo binadamu huoza na kuwa udongo. Hivyo, kuongea na mtu aliyekufa ni sawa na kuongea na udongo ukitegemea udongo huo ukusikie au uongee na wewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu zilizopandwa kwenye udongo wenye rutuba ni rahisi sana kuvamiwa na magugu iwapo mwenye bustani hataipalilia bustani yake kila siku. Kila siku tunapaswa kupalilia bustani zetu za kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu ni neno la Mungu na kudondoka kwake kwenye ardhi si mwisho wa maisha yake. Mambo kadha wa kadha yanaweza kutokea yanayoweza kuathiri ukuaji wa mbegu husika. Nyingine zinaweza kuanguka karibu na njia ndege wakaja wakazila, nyingine zinaweza kuanguka penye miamba pasipokuwa na udongo mwingi wa kutosha, nyingine zinaweza kujifukia ndani kabisa ya ardhi na kupotelea huko kwa miaka mingi, mvua inaweza kunyesha na kuhamisha baadhi ya mbegu kwa kuzisomba na maji. Lakini kwa kuwa maisha yamo ndani ya mbegu, jambo fulani litatokea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Katika karne iliyopita, wanaakiolojia waligundua mbegu za pamba na ngano katika baadhi ya makaburi waliyokuwa wakiyafukua kwa ajili ya utafiti wao wa kisayansi. Mbegu hizo, zilizokadiriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 2000 hadi 4000, zilimea na kukua zilipopandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Roho ya maisha ilikuwa bado imo ndani ya mbegu hizo, pamoja na kwamba zilikosa mvua na jua kwa zaidi ya miaka 2000.

Huu ni uthibitisho kwamba kama mbegu itapandwa, itamea na kukua kama itapandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Matumizi sahihi, watu ni ardhi na mazingira yetu na kile tunachokifanya baada ya kupanda mbegu ni neno la ukweli ambalo ndani yake kuna kanuni na mafundisho ya Mungu, ndicho kinachoathiri matumizi ya mbegu.”
Enock Maregesi