欧宝娱乐

Uvivu Quotes

Quotes tagged as "uvivu" Showing 1-6 of 6
Enock Maregesi
“Mungu anapokupa kipaji anategemea ukitumie vizuri kwa ajili ya wengine. Usipokitumia vizuri kwa ajili ya wengine, ama kwa uvivu au kwa woga, atawapa wengine wakitumia kwa ajili yako. Ukitumia vipaji vyako vizuri, Mungu atakuongezea maradufu. Yaani, ukitumia muda wako vizuri atakuongezea muda. Ukitumia nguvu zako vizuri atakuongea nguvu. Ukitumia pesa yako vizuri atakuongezea pesa. Ukitumia ukarimu wako vizuri atakuongezea ukarimu. Ukitumia maarifa yako vizuri atakuongezea maarifa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi (ubinadamu), si mimi (ubinafsi). Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano watakuwa na nguvu ya watu watano! Watakuwa na nguvu ya ziada kufanikisha malengo kama vile kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kama timu au kama mtu binafsi, kujenga jengo la ofisi, kutengeneza ziada katika masuala ya uchumi wa kampuni au nchi au wa mtu binafsi, ushindi katika kitu chochote kile, na kadhalika. Mimi ni ubinafsi. Sisi ni ubinadamu. Ubinafsi ni uvivu. Ubinadamu ni uchapakazi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mammon ni mungu wa pesa wa kuzimu anayesimamia mambo yote ya kifedha ulimwenguni. Ni miongoni mwa mashetani saba waliotupwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kutokea mbinguni akiwemo Ibilisi, Beelzebub, Asmodeus, Leviathan, Amon na Belphegor. Ibilisi ni mungu wa kiburi, Beelzebub ni mungu wa uroho, Asmodeus ni mungu wa zinaa, Leviathan ni mungu wa wivu, Amon ni mungu wa hasira na Belphegor ni mungu wa uvivu. Jukumu la mashetani hawa ni kusimamia kwa uaminifu mkubwa kutokea kuzimu dhambi kubwa saba duniani ambazo ni kiburi, uroho, zinaa, wivu, hasira, uvivu na uchoyo. Dawa ya dhambi hizo ni busara, kiasi, ujasiri, imani, haki, tumaini na upendo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi wanamwabudu Shetani. Lakini Shetani wanayemwabudu si Shetani Ibilisi aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu kuja kuudanganya ulimwengu wote. Ni Shetani roho ya mabadiliko, mabadiliko ya kweli, ya ufahamu kamilia ulimwengu huu ambamo sisi sote tunaishi. Wachawi, kwa maneno mengine, wanaabudu miungu 鈥� kama vile Inanna wa Mesopotamia, Isis wa Misri, Asherah wa Kaanani au Belus wa Assyria ambaye ndiye mungu wa kwanza kuabuadiwa kama sanamu duniani 鈥� iliyotwaliwa na Shetani tangu misingi ya ulimwengu huu kusimikwa. Dhambi aliyotenda Shetani mbinguni ni ndogo kuliko dhambi wanazotenda wachawi duniani, ijapokuwa dhambi aliyotenda Shetani haitaweza kusamehewa na ndiyo maana Shetani hataweza kuwasamehe wanadamu. Ni jukumu letu kuwaita wachawi wote kutoka Babeli na kuwaleta katika ukweli kama kweli wanayemwabudu ni Shetani Ibilisi, Shetani Beelzebub, Shetani Asmodeus, Shetani Leviathan, Shetani Mammon, Shetani Amon au Shetani Belphegor ambao ni mabingwa wa kiburi, uroho, zinaa, wivu, fedha, hasira na uvivu duniani. Wachawi hawajui, na usipojua waweza kufa bila kujua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Umoja una sisi (ubinadamu) si mimi (ubinafsi). Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano watakuwa na nguvu ya watu watano! Watakuwa na nguvu ya ziada kufanikisha malengo kama vile kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kama timu moja au kama mtu binafsi, kujenga shule ya kijiji, kutengeneza ziada katika masuala ya uchumi wa nyumbani au wa kampuni au wa nchi au wa mtu binafsi, ushindi katika jambo lolote lile, na kadhalika. Mimi ni ubinafsi. Sisi ni ubinadamu. Ubinafsi ni uvivu. Ubinadamu ni uchapakazi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mlaodikia ni mtu anayejua kwamba bustani yake ina magugu lakini anaona uvivu kwenda kuipalilia. Kinachofanya aone uvivu kwenda kuipalilia ni raha za dunia hii. Usiwe vuguvugu. Kama umeamua kuwa moto kuwa moto. Kama umeamua kuwa baridi kuwa baridi.”
Enock Maregesi