欧宝娱乐

Kifo Quotes

Quotes tagged as "kifo" Showing 1-17 of 17
Enock Maregesi
“Sabato ilianzishwa na Mungu siku ya saba ya uumbaji wake. Siku ya Sabato ni siku takatifu, iliyoko katika Amri Kumi za Mungu, ambayo hatuna budi kuitunza na kuiheshimu. Sheria ya Siku ya Sabato haikufa baada ya kifo cha Yesu Kristo msalabani kama Wakolosai wanavyodai. Wakolosai walifuata falsafa za kipagani, na walizileta falsafa hizo ndani ya mwili wa Kristo ambalo ni kanisa. 鈥楿siiamini鈥� Wakolosai 2:17. Iamini Wakolosai 2:20-23, ambapo Paulo anafundisha Mataifa jinsi ya kuitunza Sabato, na 1 Wakorintho 12:27 ambayo inatoa maana halisi ya Wakolosai 2:17. 鈥楳wili wako ni wa Kristo鈥� ni tofauti na 鈥榤wili wa Kristo鈥� na ni tofauti na kanisa. Ukiamini kama mwili wako ni wa Kristo na ni kanisa, utaitunza Sabato.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hakuna shaka yoyote (kwa mfano) kwamba mboga za majani na matunda vina vitamini nyingi mwilini na madini na vitu vyote vizuri katika mwili wa binadamu, na kwamba kadhalika vina kirutubisho cha ufumwele ambacho huzuia kufunga choo na matatizo mengine ya mfumo wa usagaji chakula. Kirutubisho hiki kikizidi mwilini utapata matatizo makubwa yatakayoweza hata kukusababishia kifo!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kufanikiwa katika maisha lazima kitu fulani ambacho si cha kawaida kitokee katika maisha yako, bila kujali uko upande wa Yesu au upande wa Shetani. Kufanikiwa katika maisha ni sawa na kwenda mbinguni, au kuishi mbinguni duniani. Kitu ambacho si cha kawaida kutokea katika maisha yako ni sawa na kifo. Fanya kitu ambacho hujawahi kufanya kupata kitu ambacho hujawahi kupata.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥�, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi.

Wanaendelea kusema kuwa baada ya 鈥楤ig Bang鈥� kutakuwepo na 鈥楤ig Crunch鈥�, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena.

Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥� ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya 鈥楤ig Crunch鈥�, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia.

Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu 鈥� badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri 鈥� sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea.

Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa 鈥榙ark matter鈥�, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo 鈥榤ultiverse鈥� au 鈥榤eta-universe鈥�.

Kuna kitu kinaitwa 鈥楬iggs boson鈥� 鈥� chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (鈥榤ass鈥�) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 鈥楤ig Bang鈥� miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa 鈥榚poch鈥� 鈥� ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥�, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni.

Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya 鈥榙ark matter鈥�, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha 鈥楽tandard Model鈥� litapatikana.

Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana 鈥楬iggs boson鈥� mwaka 1993 iliitwa 鈥楾he God Particle鈥�. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata.

Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wana uwezo wa kupeleleza hadi kipindi cha karne ya kwanza ambapo Yesu aliishi, alikufa, alifufuka na alipaa kwenda mbinguni, na wana uwezo wa kujua mambo mengi kwa hakika yaliyofanyika katika kipindi hicho na hata katika kipindi cha kabla ya hapo.

Kuna miujiza ambayo Yesu aliifanya ambayo haiko ndani ya Biblia. Kwa mfano, Biblia inasema Yesu alizaliwa ndani ya zizi la ng鈥檕mbe wakati sayansi inasema alizaliwa nje ya zizi la ng鈥檕mbe; na muujiza wa kwanza kuufanya ambao hauko ndani ya Biblia ni kutembea mara tu baada ya kuzaliwa, na watu na ndege wa angani kuganda kabla ya kuzaliwa Masihi na kabla ya wakunga kufika kumsaidia Maria Magdalena kujifungua.

Akiwa na umri wa miaka sita, sayansi inasema, Yesu alikuwa akicheza na mtoto mwenzake juu ya paa la nyumba ya jirani na mara Yesu akamsukuma mwenzake kutoka juu hadi chini na mwenzake huyo akafariki papo hapo. Watu walipomsonga sana Yesu kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mwenzake, na kwamba wangemfungulia mashtaka, Yesu alikataa katakata kuhusika na kifo hicho.

Lakini walipozidi kumsonga, aliusogelea mwili wa rafiki yake kisha akamwita na kumwambia asimame. Yule mtoto alisimama! Huo ukawa muujiza mkubwa wa kwanza wa Yesu Kristo, kufufua mtu nje ya maandiko matakatifu.

Kuna mifano mingi inayodhihirisha uwepo wa Mungu ambayo wanasayansi hawawezi hata kuipatia majibu. Tukio la Yoshua kusimamisha jua limewashangaza wanasayansi hadi nyakati za leo. Mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walijaribu kurudisha muda nyuma kwa kompyuta kuona kama kweli wangekuta takribani siku moja imepotea kama ilivyorekodiwa katika Biblia.

Cha kushangaza, cha kushangaza mno, walikuta saa 23 na dakika 20 zimepotea katika mazingira ambayo hawakuweza na hawataweza kuyaelewa. Walipochunguza vizuri walikuta ni kipindi cha miaka ya 1500 KK (Jumanne tarehe 22 Julai) ambacho ndicho tukio la Yoshua la kusimamisha jua na kusogeza mwezi nyuma digrii 10, ambazo ni sawa na mzunguko wa dakika 40, lilipotokea.

Kwa kutumia elimu ya wendo, elimu ya kupanga miaka na matukio ya Kibiblia, dunia iliumbwa Jumapili tarehe 22 Septemba mwaka 4000 KK. Hata hivyo, mahesabu ya kalenda yanaonyesha kuwa Septemba 22 ilikuwa Jumatatu (si Jumapili) na kwamba kosa hilo labda lilisababishwa na siku ya Yoshua iliyopotea.

Hayo yote ni kwa mujibu wa Profesa C. A. Totten, wa Chuo Kikuu cha Yale, katika kitabu chake cha 鈥楯oshua鈥檚 Long Day and the Dial of Ahaz: A Scientific Vindication and a Midnight Cry鈥� kilichochapishwa mwaka 1890.

Kama hakuna Mungu iliwezekanaje Yoshua aombe jua lisimame na jua likasimama kweli? Iliwezekanaje Yesu aseme atakufa, atafufuka na atapaa kwenda mbinguni na kweli ikatokea kama alivyosema? Ndani ya Biblia kuna tabiri 333 zilizotabiri maisha yote ya Yesu Kristo hapa duniani na zote zilitimia 鈥� bila kupungua hata moja. Utasemaje hapo hakuna Mungu? Mungu yupo, naamini, sijui.

Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni si la vitabu vitakatifu pekee, hata sayansi inakubaliana na hilo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu wakati anakufa msalabani hakufikiria kifo. Alifikiria maisha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kula sana ni kujichimbia kaburi kwa meno yako mwenyewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kula sana kunaweza kusababisha virutubisho kuzidi mwilini zaidi ya kiwango kinachohitajika na mwili, ambavyo baadaye vinaweza kusababisha madhara ya papo kwa hapo kama tumbo kuuma au tumbo kujaa gesi! Baada ya muda mrefu wingi wa virutubisho hivi unaweza kuingiliana na ufyonzaji wa madini kama fosforasi, kalisi, magnesi, chuma, na zinki, hali inayoweza kusababisha upungufu mkubwa wa virutubisho, unaoweza kusababisha kifo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“WWPP ('WODEA Witness Protection Programme') ni Programu Maalumu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia ya kuwakinga mashahidi wa kihalifu kwa kuwapa makazi mapya, majina mapya, kazi mpya, historia mpya ya maisha, na sura mpya, kuwakinga na Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ukivunja Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita utauwawa, tena utauwawa kinyama, wewe na familia yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni uzima wa milele. Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni Shetani. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni Yesu Kristo. Yesu Kristo ni njia iliyo huru ya kwenda mbinguni. Shetani ni njia iliyo huru ya kwenda ahera.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Askari wa Kirumi alimchoma Yesu mkuki ili andiko litimie. Askari huyo ambaye Biblia haikumtaja jina kwa sababu zilizoko nje ya uwezo wetu, alivyoona kweli amepona na ameona alishuhudia, na ushuhuda wake ulitoka moyoni, ili nasi tupate kusadiki. Wauaji wa Kirumi walipoona kwamba wale wezi waliosulubiwa pamoja na Yesu walikuwa bado hawajakata roho, waliwavunja miguu ili washindwe kupumua na hivyo kuharakisha kifo chao. Kwa upande wa Yesu, waliona alishapoteza fahamu na labda alishafariki. Kuthibitisha hilo askari wa Kirumi alirusha mkuki, nao ukatoboa utando unaozunguka moyo wa Yesu na mapafu ya Yesu, na damu na maji kutoka. Lakini yote hayo yalishatabiriwa miaka mingi kabla ya Yesu: 鈥楬akuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa鈥� na 鈥楴ao watamtazama yeye ambaye walimchoma鈥�.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna sababu za msingi na za kinabii za damu na maji vilivyotoka katika mbavu za Yesu Kristo msalabani. Ubavu wake uliochomwa na mkuki ulithibitisha kifo chake cha kibinadamu, huku vingine vyote vikitimiza unabii wake uliotajwa na Yohana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yeyote anayekufa chini ya miaka 70 ameuwawa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu asingekuwepo matajiri wangehonga kifo ili waishi milele.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ni mkubwa kuliko jumla ya matatizo yote na vitu vyote alivyoviumba na ana uwezo wa kufanya kila kitu alichosema atafanya bila kupunguza au kuongeza chochote. Usidanganywe na matatizo. Amka, kabla kifo hakijakufika.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maisha ni Dunia. Lakini Dunia ni basi. Sisi ni wasafiri. Mtu anapokufa amefika mwisho wa safari yake, huku Dunia ikiendelea.”
Enock Maregesi