欧宝娱乐

Jua Quotes

Quotes tagged as "jua" Showing 1-11 of 11
Enock Maregesi
“Hasira ni Shetani. Hekima ni Mungu. Kila kitu kimo ndani yetu. Hasira imo ndani yetu. Hekima imo ndani yetu. Atomu ni matofali ya ujenzi wa kila kitu ulimwenguni likiwemo jua na miili ya wanadamu. Ndani ya atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi. Kama miili yetu imetengenezwa na atomu na katika kila atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi, hivyo basi, tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mazuri na tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mabaya. Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana. Geuza hasira yako kuwa hekima kwa faida yako na kwa faida ya wengine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitaka kumjua mwanamke jua historia yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥�, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi.

Wanaendelea kusema kuwa baada ya 鈥楤ig Bang鈥� kutakuwepo na 鈥楤ig Crunch鈥�, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena.

Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥� ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya 鈥楤ig Crunch鈥�, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia.

Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu 鈥� badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri 鈥� sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea.

Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa 鈥榙ark matter鈥�, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo 鈥榤ultiverse鈥� au 鈥榤eta-universe鈥�.

Kuna kitu kinaitwa 鈥楬iggs boson鈥� 鈥� chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (鈥榤ass鈥�) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 鈥楤ig Bang鈥� miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa 鈥榚poch鈥� 鈥� ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa 鈥楤ig Bang鈥�, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni.

Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya 鈥榙ark matter鈥�, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha 鈥楽tandard Model鈥� litapatikana.

Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana 鈥楬iggs boson鈥� mwaka 1993 iliitwa 鈥楾he God Particle鈥�. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata.

Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wana uwezo wa kupeleleza hadi kipindi cha karne ya kwanza ambapo Yesu aliishi, alikufa, alifufuka na alipaa kwenda mbinguni, na wana uwezo wa kujua mambo mengi kwa hakika yaliyofanyika katika kipindi hicho na hata katika kipindi cha kabla ya hapo.

Kuna miujiza ambayo Yesu aliifanya ambayo haiko ndani ya Biblia. Kwa mfano, Biblia inasema Yesu alizaliwa ndani ya zizi la ng鈥檕mbe wakati sayansi inasema alizaliwa nje ya zizi la ng鈥檕mbe; na muujiza wa kwanza kuufanya ambao hauko ndani ya Biblia ni kutembea mara tu baada ya kuzaliwa, na watu na ndege wa angani kuganda kabla ya kuzaliwa Masihi na kabla ya wakunga kufika kumsaidia Maria Magdalena kujifungua.

Akiwa na umri wa miaka sita, sayansi inasema, Yesu alikuwa akicheza na mtoto mwenzake juu ya paa la nyumba ya jirani na mara Yesu akamsukuma mwenzake kutoka juu hadi chini na mwenzake huyo akafariki papo hapo. Watu walipomsonga sana Yesu kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mwenzake, na kwamba wangemfungulia mashtaka, Yesu alikataa katakata kuhusika na kifo hicho.

Lakini walipozidi kumsonga, aliusogelea mwili wa rafiki yake kisha akamwita na kumwambia asimame. Yule mtoto alisimama! Huo ukawa muujiza mkubwa wa kwanza wa Yesu Kristo, kufufua mtu nje ya maandiko matakatifu.

Kuna mifano mingi inayodhihirisha uwepo wa Mungu ambayo wanasayansi hawawezi hata kuipatia majibu. Tukio la Yoshua kusimamisha jua limewashangaza wanasayansi hadi nyakati za leo. Mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walijaribu kurudisha muda nyuma kwa kompyuta kuona kama kweli wangekuta takribani siku moja imepotea kama ilivyorekodiwa katika Biblia.

Cha kushangaza, cha kushangaza mno, walikuta saa 23 na dakika 20 zimepotea katika mazingira ambayo hawakuweza na hawataweza kuyaelewa. Walipochunguza vizuri walikuta ni kipindi cha miaka ya 1500 KK (Jumanne tarehe 22 Julai) ambacho ndicho tukio la Yoshua la kusimamisha jua na kusogeza mwezi nyuma digrii 10, ambazo ni sawa na mzunguko wa dakika 40, lilipotokea.

Kwa kutumia elimu ya wendo, elimu ya kupanga miaka na matukio ya Kibiblia, dunia iliumbwa Jumapili tarehe 22 Septemba mwaka 4000 KK. Hata hivyo, mahesabu ya kalenda yanaonyesha kuwa Septemba 22 ilikuwa Jumatatu (si Jumapili) na kwamba kosa hilo labda lilisababishwa na siku ya Yoshua iliyopotea.

Hayo yote ni kwa mujibu wa Profesa C. A. Totten, wa Chuo Kikuu cha Yale, katika kitabu chake cha 鈥楯oshua鈥檚 Long Day and the Dial of Ahaz: A Scientific Vindication and a Midnight Cry鈥� kilichochapishwa mwaka 1890.

Kama hakuna Mungu iliwezekanaje Yoshua aombe jua lisimame na jua likasimama kweli? Iliwezekanaje Yesu aseme atakufa, atafufuka na atapaa kwenda mbinguni na kweli ikatokea kama alivyosema? Ndani ya Biblia kuna tabiri 333 zilizotabiri maisha yote ya Yesu Kristo hapa duniani na zote zilitimia 鈥� bila kupungua hata moja. Utasemaje hapo hakuna Mungu? Mungu yupo, naamini, sijui.

Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni si la vitabu vitakatifu pekee, hata sayansi inakubaliana na hilo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna vitu vitatu ndani ya mtu: kuna hiari, kuna ufahamu, na kuna mwili. Hiari inatawaliwa na Mungu; ufahamu unatawaliwa na malaika mwema; mwili unatawaliwa na nyota lakini chini ya usimamizi wa malaika wema: malaika wema walisimamisha jua na mwezi kwa ajili ya Yoshua na wana wa Israeli juu ya Gibeoni na katika bonde la Aiyaloni, walirudisha jua nyuma kwa ajili ya Hezekia mfalme wa Yuda na kwa ajili ya nabii Isaya, na waliifanya dunia 鈥榢uvaa koti鈥� ghafla wakati wa kusulubiwa kwa Mwanakondoo wa Mungu Anayeondoa Dhambi. Moyoni ni mahali patakatifu. Hata malaika wema hawawezi kuona ndani ya moyo wa mtu, ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kufanya hivyo, na alichokihifadhi Mungu ndani ya moyo huo ni hiari ya mtu ya kuchagua mema au mabaya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dunia huzunguka kwenye mhimili wake na huzunguka jua. Jua huzunguka kwenye mhimili wake na huzunguka falaki. Dunia hutumia takriban siku moja kuzunguka kwenye mhimili wake, na hutumia takriban mwaka mmoja kuzunguka jua. Jua hutumia takriban siku ishirini na tano kuzunguka kwenye mhimili wake, na hutumia takriban miaka milioni mia mbili na hamsini kuzunguka falaki. Yoshua alisimamisha jua ili lisizunguke kwenye mhimili wake na lisizunguke falaki. Kwa sababu jua lilisimama, kila kitu kilichoathiriwa na jua hilo kilisimama pia ikiwemo dunia. Hata hivyo, kwa sababu tukio la Yoshua kusimamisha jua na mwezi yalikuwa maajabu kutoka kwa malaika wema, malaika wema ndiyo wanaojua kwa hakika nini kilitokea. Yoshua alikuwa sahihi kusema jua lisimame si dunia isimame. Mungu aliweza kusimamisha jua kwa ajili ya Yoshua kuwashinda maadui zake, kwa sababu aliamini. Mungu anaweza kusimamisha jua kwa ajili yako kuwashinda maadui zako, ukiamini. Mungu anapokuwa na wewe matatizo yako yako matatizoni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Falaki maana yake ni kundi la nyota na sayari ikiwemo dunia. Falaki yetu inaitwa Njiamaziwa, 鈥榯he Milky Way galaxy鈥�, yenye mabilioni ya mifumo ya jua ukiwemo wa kwetu. Mungu alisimamisha jua katika falaki ya Njiamaziwa kwa ajili ya Yoshua, ili apate muda wa kutosha kuwashinda maadui zake 鈥� wanajeshi wa mataifa matano. Kila mtu alishangaa sana kipindi hicho. Kila mtu anashangaa sana kipindi hiki. Mungu akikubariki watu watasema wewe ni mchawi. Hawatajua nini kilitokea. Kwani kwa Mungu hakuna kinachoshindikana. Mungu aliweza kutenda miujiza kwa ajili ya Yoshua, na kwa ajili ya wana wa Israeli huko Gibeoni na huko Aiyaloni, anaweza kutenda miujiza kwa ajili yako popote pale ulipo. Mungu anachotaka kutoka kwako ni imani ya kweli juu yake, kwa mwili na kwa roho yako yote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sayari yetu hujulikana kama Dunia na jua letu hujulikana kama Sol. Dunia imo ndani ya mfumo wa jua wa Sol. Mfumo wa jua wa Sol umo ndani ya mfumo wa jua wa Sol Sector au Solar Interstellar Neighborhood, kwenye wenzo wa Orion wa falaki ya Njiamaziwa, wenye mifumo ya jua zaidi ya 40 ikiwemo Alpha Centauri, Nemesis, Procyon na Sirius. Solar Interstellar Neighborhood imo ndani ya falaki ya Njiamaziwa yenye nyenzo nne zinazozunguka kwa pamoja na falaki nzima. Falaki ya Njiamaziwa imo ndani ya kishada (鈥榗luster鈥�) chenye zaidi ya falaki 55 ikiwemo Andromeda, Leo A, M32 na Triangulum, kinachojulikanacho kama 鈥榯he Local Galactic Group鈥�. 鈥楾he Local Galactic Group鈥� imo ndani ya mfumo wa kishada kikubwa zaidi kiitwacho Virgo Supercluster, chenye makundi zaidi ya 100 ya falaki. Virgo Supercluster imo ndani ya mfumo mwingine mkubwa zaidi wa vishada uitwao Laniakea (Local Supercluster) wenye vishada zaidi ya 500 vya falaki. Hapo ndipo mwisho wa ulimwengu wetu unaoweza kuonwa na wanasayansi wetu. Kutoka duniani mpaka Laniakea ni umbali wa kilometa bilioni trilioni 250, miaka bilioni 13.8 iliyopita.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wanaamini kuwa Yesu atarudi tarehe 29 Julai 2016. Tarehe hiyo kitu kikubwa sana kitatokea katika dunia yetu kitakachosababisha tetemeko kubwa la ardhi, litakalosababishwa na kubadilika kwa ncha za dunia, tendo litakalosababisha mionzi ya gama kutoka kwenye jua ifike duniani na kuua kila kitu kinachoonekana katika uso wa dunia hii. Watakatifu watafufuka na kumlaki Kristo mawinguni, ambaye anakuja kuwachukua wateule na kumweka Shetani kifungoni kwa miaka 1000. Hayo yote, wanasema, yatatokea ndani ya siku 11 kuanzia leo. Yaani, kusini mwa dunia kutakuwa kaskazini mwa dunia, kaskazini mwa dunia kutakuwa kusini mwa dunia.

Kitendo hicho kitafanya dunia ikose kinga ya sumaku iitwayo 鈥榤agnetosphere鈥� ambayo hukinga dunia dhidi ya mionzi ya gama kutoka kwenye jua. Mionzi hiyo hugonga ukuta wa 鈥榤agnetosphere鈥� kila baada ya dakika 8 kwa mwendokasi wa kilometa milioni 1080 kwa saa; na kusambazwa katika ncha za dunia ambapo aghalabu huchanganyikana na oksijeni na kutengeneza kitu kinaitwa 鈥榓urora鈥�, au mwanga wa ncha, ambacho ni maajabu mengine ya angani. Mwaka 2012 wanasayansi walisema ncha za dunia zingebadilika lakini hazikubadilika. Je, muda umefika sasa wa kuwaamini wanasayansi? Biblia ni chuo cha Mungu. Soma Biblia kupata maarifa.”
Enock Maregesi