ŷ

Dunia Quotes

Quotes tagged as "dunia" Showing 91-120 of 124
Enock Maregesi
“Jina langu ni Enock Maregesi na ningependa kukwambia kisa kidogo kuhusiana na bibi yangu, Martha Maregesi. Mwanamke huyu alikuwa mke mwenye upendo usiokuwa na masharti yoyote. Alikuwa mama na bibi aliyefundisha familia yake umuhimu wa kujitolea na umuhimu wa uvumilivu. Ijapokuwa hakupendelea sana kujizungumzia mwenyewe, ningependa kukusimulia kisa kidogo kuhusiana na hadithi ya maisha ya mwanamke huyu wa ajabu katika maisha yangu.

Bibi yangu alizaliwa katika Kitongoji cha Butimba, Kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi, Tarafa ya Nyanja (Majita), Wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, katika familia ya watoto kumi, mwaka 1930. Alisoma katika Shule ya Msingi ya Kome ambako alipata elimu ya awali na msingi na pia elimu ya kiroho kwani shule yao ilikuwa ya madhehebu ya Kisabato. Aliolewa na Bwana Maregesi Musyangi Sabi mwaka 1946, na kufanikiwa kupata watoto watatu; wa kiume wakiwa wawili na wa kike mmoja. Matatizo hasa ya bibi yalianza mwaka 2005, alipougua kiharusi akiwa nyumbani kwake huko Musoma. Hata hivyo alitibiwa hapo Musoma na Dar es Salaam akapona na kuwa mwenye afya ya kawaida. Lakini tarehe 19/10/2014 alipatwa tena na kiharusi na kulazwa tena katika Hospitali ya Mkoa ya Musoma, ila akajisikia nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani � lakini kwa maagizo ya daktari ya kuendelea na dawa akiwa nje ya hospitali. Tarehe 29/10/2014 alirudi tena Hospitali ya Mkoa ya Musoma kwa tiba zaidi, lakini tarehe 4/11/2014 saa 7:55 usiku akafariki dunia; akiwa amezungukwa na familia yake.

Dunia ina watu wachache sana wenye matumaini na misimamo ya kutegemea mazuri, na wachache zaidi ambao wako tayari kugawa matumaini na misimamo hiyo kwa watu wengine. Nitajisikia furaha siku zote kwamba miongoni mwa watu hao wachache, hata bibi yangu alikuwemo. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake. Kwa kuwa bibi yangu ametanguliwa na msalaba, msalaba utamwongoza mahali pa kwenda.”
Enock Maregesi

“... di dunia ini ada beberapa hal yang tidak bisa diubah: manusia-manusia yang hidup di masa lalu. Manusia-manusia yang memilih untuk tinggal dalam kenangan dan menutup mata pada kenyataan.”
Devania Annesya, Muara Rasa

“Ada hal-hal yang ingin aku lupakan � saat -saat di mana aku merasa dunia tidak adil dan tak ada seorang pun yang menuntut keadilan untukku.”
Devania Annesya, Februari: Ecstasy

“Berkata Isa alaihi-salam seterusnya: Amat heran keadaan kalian semua. Kalian bekerja kuat untuk dunia, padahal kalian mendapat bahagian kalian dari rezeki, meskipun kalian tidak bekerja. Tetapi kalian tidak bekerja kuat untuk akhirat, padahal kalian tidak akan mendapat bahagian kalian dari pahala, melainkan dengan beramal.”
عبد الله بن علوي بن حداد الشافعي, Penuntun Hidup Bahagia

“Andra, cewek macam Ariel itu, sekali kamu taklukkan dia, dia akan menaklukkan seluruh dunia untukmu. Tapi kalau kau sampai gagal menaklukkannya, dia yang akan menaklukkanmu!”
Devania Annesya, X: Kenangan yang Berpulang

“Hal yang paling menyedihkan di dunia ini adalah... ketika manusia harus mencuri hanya untuk bertahan hidup.”
Devania Annesya, Queen: Ingin Sekali Aku Berkata Tidak

Enock Maregesi
“Usiwe na wasiwasi, Peter. Hizo ni hisia zangu tu. Huwezi kuwa mpelelezi. Lakini, kusema ule ukweli, ningependa sana kuonana na John Murphy. Kuna kazi binafsi ningependa kumpa. Wewe unatoka Afrika, hujawahi kumwona?� Debbie alizidi kumshtua Murphy.
“Nani?� Murphy aliuliza huku akitabasamu.
“John Murphy wa Afrika.�
“Sijawahi kumwona. Mbona unamuulizia hivyo?�
Debbie alitulia. Kisha akarusha nywele ili aone vizuri.
“Nampenda sana!�
“Kwa nini?�
“Simpendi kwa mahaba, lakini.�
“Ndiyo. Kwa nini?�
“OK. Nampenda kwa kipaji chake. Alichopewa na Mungu, cha ujasusi. Kusaidia watu.�
“Ahaa!� Murphy alidakia, sasa akifikiri sana.
“Murphy ana mashabiki wengi hapa Meksiko bila yeye mwenyewe kujua, kwa sababu ya kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya � hasa wa huku Latino. Tatizo lake haonekani. Wengi hudhani ni hadithi tu, kwamba hakuna mtu kama huyo hapa duniani.�
“Hapana! Murphy yupo! Ni mfanyabiashara maarufu huko Tanzania. Lakini ndiyo hivyo kama unavyosema ... Haonekani!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

“Cinta saja tidak cukup. Sebenarnya dunia ini tidak mengenal kata cukup.”
Devania Annesya, Elipsis

“Ada sesuatu di dunia ini yang tidak perlu dipikirkan alasannya, mengapa dan bagaimana. Kalaupun ada kehidupan setelah ini, saya masih akan melakukan kebodohan yang sama. Saya akan tetap mencintai Atran.”
Devania Annesya, Elipsis

“Karena aku tidak mau dilupakan. Aku ingin selalu diingat oleh dunia. Terutama... olehmu.”
Devania Annesya, X: Kenangan yang Berpulang

Enock Maregesi
“Mpenzi. Sikiliza. Magaidi yaliyomuua Marciano yana mtandao dunia nzima na watu wote wanayajua. Yanaitwa Kolonia Santita. Tatizo hata hivyo ni moja: Hakuna mtu amewahi kuthibitisha au kutoa ushuhuda wa uhalifu wao ili watiwe nguvuni. Huendesha maisha yao kibabe na yana kila mbinu ya kukwepa sheria, ndani na nje ya Meksiko. Watu wengi wameuwawa kwa sababu ya Kolonia Santita. Ukileta kidomodomo yanakuua; au yanakupa notisi ya kuhama mji au nchi, ukakae mbali na Meksiko au Mexico City.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kila binadamu hapa duniani ni wa thamani kubwa. Chochote utakachofanya, kizuri au kibaya, kidogo au kikubwa, kitabadilisha maisha ya watu. Ukiwa na msingi mzuri kwa mwanao ataishi vizuri atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mkubwa wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Ukiwa na msingi mbaya kwa mwanao ataishi vibaya atakapokuwa mkubwa, atakuwa na uwezo mdogo wa kuacha dunia katika hali nzuri kuliko alivyoikuta. Kuwa mkarimu kwa mazingira, kuwa mkarimu kwa wanyama, kuwa mkarimu kwa binadamu wenzako, kwa faida ya vizazi vijavyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.”
Enock Maregesi

“Tapi bukankah setiap energi di dunia ini tidak akan pernah hilang? Ia hanya akan bertransformasi dalam bentuk yang lain.”
Devania Annesya, Elipsis

“Aku ingin kau belajar satu hal, di dunia ini ada sesuatu yang kau inginkan namun tak bisa kau dapatkan.”
Devania Annesya, Queen: Ingin Sekali Aku Berkata Tidak

“Akal pikiran Maharaja Dunia, Allah Maharaja Bumi dan Langitnya.”
Gatot Soedarto

“Telah berkata Muhammad bin Sirin: Dua orang lelaki telah bersengketa mengenai sepotong tanah, lalu Allah mewahyukan kepada bumi itu supaya berbicara kepada kedua-duanya. Maka bumi pun berkata kepada mereka: Wahai kalian yang bodoh! Sebenarnya aku sebelum kalian berdua telah dimiliki oleh seribu orang yang cacat matanya, apatah lagi oleh orang-orang yang celek dan sihat seperti kamu berdua ini.”
عبد الله بن علوي بن حداد الشافعي, Penuntun Hidup Bahagia
tags: dunia

“Setengah para salaf berdoa: Wahai Tuhan yang menahan langit supaya tidak runtuh ke atas bumi, kecuali dengan izinNya! Tahanlah dunia supaya tidak datang kepadaku.”
عبد الله بن علوي بن حداد الشافعي, Penuntun Hidup Bahagia
tags: dunia

Enock Maregesi
“Kolonia Santita imesambaa dunia nzima. Hapa Meksiko wana magenge rafiki zaidi ya mia moja yakiwemo makubwa kabisa katika Latino ya Matamolos na Baja California. Nikitekwa nyara na memba yoyote wa magenge hayo, kuna uwezekano mkubwa wasinifanye chochote au nisilipe chochote kwa sababu ya Wanda. Fadhila ya uhalifu. Kwa sababu ya fadhila ya uhalifu; baba, au viongozi wengine wa serikali ambao watoto wao wamo ndani ya 'mpango' huo, wanatakiwa wawakingie kifua (kwa namna yoyote wanayoweza) pindi wanapoanguka katika mikono ya dola na sheria. Wasipofanya hivyo kutakuwa na vita ya ndani kwa ndani � kama unanielewa. Hivyo, kuna mtu anaitwa El Tigre � baba yake Wanda � ndiye ninayetaka unisaidie. Amemuua Marciano, na watu wengi wa Meksiko. Nataka kumlipia kisasi Marciano, na marafiki zangu wengi ambao El Tigre amewaua, hata kwa njia isiyodhahiri.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru, alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya Dunia, na kutafuta kupitia maabara za CERN ('Conseil Européen pour la Recherche Nucléaire') chembe ndogo ya 'higgs' ('Higgs Boson') inayosemekana kuhusika na uzito ('mass') wa chembe ndogo kumi na sita za atomu kasoro chembe ya mwanga; iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 'Big Bang', miaka bilioni kumi na tatu nukta saba iliyopita kwa faida ya uanadamu.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Ford Bronco ilikuwa sehemu ya upelelezi wa polisi wa Tume ya Dunia, na ilipigwa mnada baada ya upelelezi na kesi kumalizika. Kiasi kikubwa cha pesa iliyopatikana kilikwenda kwa WPD � Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia � ili iendelee kuimarisha huduma ya kukomesha biashara haramu ya madawa ya kulevya duniani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watoto hawatakiwi kuchungwa kupita kiasi hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho. Uhuru utakaowanyima wakiwa wadogo watakuja kuutafuta baadaye wakiwa wakubwa. Wakiutafuta baadaye wakiwa wakubwa hawataeleweka vizuri katika jamii. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata lakini si uhuru wa kila kitu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu alimpa kila mmoja wetu vipawa na vipaji vya pekee kwa ajili ya huduma yake. Kazi yake kwetu hapa duniani ni kutumia vipawa na vipaji vyetu kwa ajili ya huduma ya watu wengine. Kila mmoja wetu ana kitu fulani anachoweza kutoa kwa ajili ya mtu mwingine mwenye shida. Tunaweza kutoa pesa zetu na muda wetu kwa watu maskini. Tunaweza kuwa marafiki kwa watu wapweke au watu wasiojiweza kiafya. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea kwa ajili ya mabadiliko ya watu wengine. Tunaweza kuwa wasuluhishi wa migogoro ya amani. Tunaweza kuwa na upendo usiokuwa na masharti yoyote kwa familia zetu. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea au kazi za kuajiriwa kwa uadilifu, uaminifu, heshima, na upendo kwa wengine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kila mmoja wetu ana kitu cha kutoa. Wengine wana pesa, wengine wana vipaji, wengine wana muda. Vipaji vyote tulivyopewa na Mungu, vikubwa au vidogo, hatuna budi kuvitumia kiukarimu kwa watu wanaovihitaji. Tunapofanya hivyo tunaleta mabadiliko katika dunia kwa ajili ya watu fulani, na tunapata maana halisi ya maisha na toshelezo la moyo katika maisha yetu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kila mtu kabla ya kuzaliwa alipewa na Mwenyezi Mungu unabii na nyota ya ufalme. Una bahari ya fursa ya kuwa kitu chochote unachotaka kuwa katika dunia hii. Kama unataka furaha, furaha iko ndani yako. Kama unataka utajiri, utajiri uko ndani yako. Kama unataka amani, amani iko ndani yako. Kama wewe ni tone na fursa ni bahari, wewe ni bahari ndani ya tone.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unabii ni uwezo alionao mtu wa kuongea mambo matakatifu ya Mungu, kuwaongoza wenzake katika njia njema. Mungu humwambia nabii kitu cha kusema na nabii huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Mungu hawezi kuongea na watu mpaka watu wajue jinsi ya kuongea naye, na wakati mwingine ni rahisi sana kusikia ujumbe kutoka kwa mtu kuliko kuusikia ujumbe huo moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Mungu anaweza kukwambia useme kitu fulani kwa mtu au watu fulani. Unaweza usijue kwa nini anakwambia ufanye hivyo, lakini utajisikia msukumo wa hali ya juu wa kutangaza ujumbe uliopewa kuuwasilisha. Mungu hatakulazimisha, lakini atakung’ang’aniza, na ni Mungu pekee anayejua lengo la mawasiliano hayo. Mungu akikwambia ufanye kitu fanya mara moja, usiulize kwa nini. Kazi yako ni kufanya unachotakiwa kufanya, kusema unachotakiwa kusema, si kuuliza maswali. Mtumie rafiki yako wa kiroho kukuongoza katika mema na mabaya, na usitambe � kwamba unaongea maneno uliyoambiwa na Mungu uyaongee. Ukiwa na uwezo mkubwa wa kuongea na Mungu utaleta mabadiliko katika dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Radia hakuwa na makosa. Wengi huishi maisha yao bure. Yeye aliishi ya kwake kwa ajili ya watu. Hakuishi tu kama raia wa Tunisia. Aliishi kama raia wa uanadamu, maadili mema na uchapakazi. Watu walimsifu kwa kuwa na kaulimbiu ya 'Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta'.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Hufanani na yoyote katika dunia hii. Unafanana na wewe mwenyewe. Usimdharau mtu, humjui!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kutakuwepo na nguvu za chanya na hasi katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu moyo wako kuwa chanya utakuwa chanya. Ukiruhusu moyo wako kuwa hasi utakuwa hasi. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako mpaka wewe mwenyewe umwonyeshe. Ukionyesha chanya Mungu atakupa chanya. Ukionyesha hasi Shetani atakupa hasi.”
Enock Maregesi